Wednesday, August 21

Serikali yatoa baraka Shindano la Miss Tanzania

0


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na naibu wake Juliana Shonza wamekutana na waandaaji wapya wa shindano la Miss Tanzania ambao ni kampuni ya The Look wakiongozwa na mkurugenzi wake Basilla Mwanukuzi pamoja na kamati yake kuzungumzia maandalizi ya uzinduzi wa shindano hilo utakaofanyika Aprili 7 mwaka huu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea mpango mkakati wa Mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi ambaye sasa ndiye muendeshaji wa Mashindano hayo. Serikali imetoa baraka zake kwa uongozi wa The Look Company Limited kwa nia yake ya kurudisha heshima, hadhi na mvuto wa tasnia ya urembo hapa nchini kupitia Mashindano hayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) na Naibu wake, Juliana Shonza (kushoto) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi baada ya mazungumzo yao, jana katika ofisi za Ukombozi wa bara la Afrika, zilizopo Garden avenue, Jijini Dar es salaam.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.