Monday, August 19

Rais Magufuli ataja sababu ya deni la Taifa kuongezeka

0


Baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG Profesa Mussa Assad kuishauri serikali idhibiti ukuaji wa deni la taifa ambalo limekuwa kwa asilimia 12 kutoka trilioni 41 iliyokuwa mwaka jana hadi trilioni 46 mwaka huu wa fedha. 

Rais John Magufuli amefafanua sababu za ukuaji wa deni hilo, ambapo amesema fedha hizo zimekopwa kwa ajili ya kuendesha miradi ya maendeleo ambayo hapo baadae itailetea faida nchi kwa kuwa na uchumi imara usiotegemea mikopo.

“Tanzania tuna gap kubwa ya kukopa lakini uangalie unakopa kwa ajili ya nini, ukikopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ili badaae uzalishe hela usikope tena hicho ni kitu kizuri, ukikopa kitu kwa ajili ya miradi mikubwa kama ya umeme na miradi mingine mingi mikubwa inafaida kubwa kwenye uchumi,” amesema.

Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa, miradi mikubwa inayotekelezwa sasa haitegemei fedha za mikopo na kwamba kufuatia hali hiyo kuna benki kubwa takribani sita zinataka kuikopesha serikali kutokana na uchumi wa nchi kuendelea vizuri.

“Miradi mingi tunayoiendesha hadi sasa hivi hela yake ipo hatutakopa, mradi wa Standard gauge  hatujakopa lakini walipoona hawa wakopeshaji tumeaanza kujenga bila kuomba hela, kuna kampuni sita za mabenki wanataka kutukopesha. Zamani walikuwa wanaringa wanaweka riba mpaka asilimia saba hadi kumi, sasa hivi wanashuka hadi chini ya asilimia 3. Tuna ringa, fedha za iradi ipo ununuzi wa ndege tumetoa wenyewe, tunaendelea vizurii watakajua,” amesema na kuongeza.

“Tuna akiba ya fedha zinazoweza kuhimili kwa zaidi ya miezi mitano hadi sita, uchumi wetu uko vizuri, ndiyo maana ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakuwa vizuri katika nchi tano za Afrika, tumekuwa wa tatu kwa kukua kwa asilimia 6.8 na kuendelea. Wengine wanaotuzunguka hawatufikii huko.” 

Na Regina MkondeRead More

Share.

About Author

Comments are closed.