Saturday, August 17

Kesi ya Tido Mhando yapigwa kalenda

0


Kesi ya utumiaji vibaya madaraka, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Tido Mhando imehairishwa hadi Februari 28, 2018.

Kesi hiyo imeairishwa baada ya wakili upande wa utetezi, Ramadhan Maleta kuomba muda wa kupitia maelezo ya awali (PH) waliyopewa leo Februari 23, 2018 na upande wa Jamhuri kupitia wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai. 

Kesi hiyo ilitakiwa kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa, ambapo aliiarisha baada ya kukubali ombi la upande wa utetezi na kuipanga kusikilizwa tarehe 28 mwezi huu.

Hata hivyo, Hakimu Nongwa amesema dhamana ya Tido inaendelea hadi tarehe Februari 28 mwaka huu atakaporejea tena mahakamani hapo. 

Tido alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na TAKUKURU akikabiliwa na mashitaka matano, ambapo manne kati ya hayo ni ya kutumia madaraka vibaya na moja ni la kuisababishia serikali hasara ya Sh. milioni 887.1.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.