Thursday, August 22

Canada yaiachia ndege ya ATCL, kutua nchini mwaka huu

0


Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) iliyokuwa inazuiliwa nchini Canada imeachiliwa na itawasili nchini wakati wowote kuanzia sasa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa amethibitisha.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Msigwa ameandika kuwa pamoja na ndege hiyo kutua nchini mwaka huu, pia zitakuja ndege zingine tatu, mbili Bombardier CS300 na moja Boeing 787-8 Dreamliner.

“Ndege yetu aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada ilikwishaondoka Canada kuja Tanzania,” amendika Msigwa na kuongeza.

“Aidha, ndege kubwa nyingine 3 (2 Bombardier CS300 kutoka Canada & 1 Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Marekani) zitawasili baadaye mwaka huu.”Read More

Share.

About Author

Comments are closed.