Thursday, August 22

Bosi STAMICO afanya mazungumzo na Dkt. Abbasi kuhusu utoaji wa taarifa

0


Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) Mhandisi John Nayopa amekutana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dakta Hassan Abbasi, ambaye alifika katika Ofisi za Makao Makuu ya STAMICO jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamia na naye nakuzungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano katika upashanaji habari za STAMICO kwa Watanzania.

Viongozi hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika sualazima la kuelimisha Watanzania kuhusu shughuli za STAMICO kwa kutumia mitandao ya kijaamii (Social Media) ya Idara ya Habari Maelezo, Jarida la Nchi yetu linaloratibiwa na  Idara hiyo na Vyombo vya Habari kwa ujumla.

Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dakta Abbasi amesema Idara yake iko tayari kutoa mafunzo kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa STAMICO katika maeneo mbalimbali kulingana na mahitaji yao, ilikuwajengea uwezo zaidi katika taaluma zao.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akitoa maelezo kwa ufupi kuhusu Jarida la NchiYetu toleo la Novemba 2017 kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

“Kulingana na ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Idara yangu inaweza kutoa mafunzo ya kuanzia kwa wataalamu wako kuhusu Sayansi ya Mitandao ya Kijamii na uendeshaji wake; Mawasiliano kwa Umma wakati wa Majanga (Crisis Communication);pamoja na Sera na Miongozo ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii,” alifafanua Dakta Abbasi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Nayopa amemshukuru Dakta. Abbasi kwa kumtembelea ofisini kwake na ameahidi kuimarisha ushirikiano na Idara ya Habari Maelezo katika kuelimisha Watanzania kuhusu mchango wa STAMICO katika kuleta matokeo chanya kwenye Serikali ya awamu ya tano.

Na Koleta Njelekela, STAMICORead More

Share.

About Author

Comments are closed.