Tuesday, August 20

Boko Haram wavamia tena shule ya wasichana nchini Nigeria

0


Wanamgambo wa Boko Harama wamevamia shule ya wasichana iliyopo kwenye mji wa Dapchi jimbo la Yobe na kuanza kufyatua risasi na kulipua vilipuzi.

Taarifa zinasema kuwa, baada ya kusikika kwa milio hiyo, wanafunzi na waalimu waliokuwepo kwenye shule hiyo walianza kukimbia na kufanikiwa kuwatoroka wanamgambo hao.

Wakazi wa Dapchi walisema baada ya Boko Haram kukuta shule haina watu, walianza kupora, inagawa baadae vikosi vya Jeshi la Nigeria vikisaidiwa na ndege za jeshi vilifanikiwa kuzima shambulizi hilo.

Inasemekana lengo la Boko Haram lilikuwa ni kuteka tena wanafunzi hao kama ilivyofanya mwezi Aprili mwaka 2014 ambapo waliteka nyara wasichana wa shule takribani 270 katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.