Sunday, August 25

Zlatan Apigana Uwanjani, adai anampenda Mama kuliko Baba

0


Sehemu ya pili

Hii ni makala inayozungumzia maisha ya Zlatan

Aliishi na Mama yake Bi Jurka Gravic baada ya kutalakiana na baba yake mzee Sefik. Sheria zilimpa mama yake jukumu hilo kutokana na umri wa Zlatan wakati mama yake anaachana na baba yake.

Familia ni sehemu furaha pekee ya kudumu hupatikana.

Hakuwahi kufurahia Maisha ya familia, imemuumiza mara kadhaa. Aliathirika sana kisaikolojia kwa Ukosefu wa malezi mazuri ya wazazi wake (mama na Baba wa Kambo). Ugomvi kwa wazazi wa pande zote (baba yake mzazi dhidi ya Mama, Baba yake mzazi dhidi ya Baba wa kambo) ulichukua sehemu kubwa katika maisha ya kila siku ya Zlatan.

Kuishi na baba wa kambo kulimuumiza sana kwa kukosa malezi ya baba mzazi. Uzito wake ulidorora mno kutokana na kukosekana kwa lishe. Baba yao wa kambo aliitesa sana familia.

Afya yake iliimarika baada baba yake kurudi kijijin kwao kwani alikuwa akimjali sana. Katika kipindi hiki furaha ya Zlatan ilirudi kwa kiasi kikubwa na afya yake ilineemeka. Zlatan anakiri waziwazi kuwa alikuwa akimpenda zaidi baba yake kuliko mama.

Katika historia ya maisha yake hawezi kabisa kumsahau baba yake wa kumzaa. Anasema siku moja baba yake Mzee Sefik Ibrahimovic; alipata kiasi kidogo cha fedha na kwenda kumnunulia mwanae kitanda. Kwa bahati mbaya walikosa fedha za kukisafirishia. Walichukua uamuzi wa kukibeba mgongoni hadi nyumbani umbali wa kilometa 17. Mwenyewe anasema hawezi kabisa kuisahau siku hiyo.

Aliongeza kuwa siku moja baba yake alipokea mshahara, akaamua kumpa mshahara wote mwanae. Kitendo kile kilimuumiza sana Zlatan kwakuwa baba yake hakuwa na makazi maalumu na alikuwa hata akishinda njaa ilimradi tu mwanae afurahi. Vita vya Balkani viliharibu makazi ya baba yake nae akabaki kuwa mzururaji tu maisha ya baba yake pia yalimtia sana uchungu.

Baba yake alitoweka tena na alikaa kipindi kirefu bila kurudi kuiona familia baada ya kupishana kauli na baba wa kambo. Katika kipindi hiki maisha ya Zlatan yalibadilika sana, alichanganyikiwa kiasi cha kudhohofu mwili na aliachana kabisa na shule. Hata siku za Mitihan alikuwa haende shule hivyo aliamua kwenda kwenye shule za Kung Fu.

Madawa ya kulevya, bangi na pombe vilitawala sana kijijini kwao. Kwenye kitabu chake aliandika na kusema soka liliokoa maisha yake.

Safari ya Zlatan Malmo FF
Zlatan alipita kipindi kigumu sana kwenye akademi ya Malmo FF. Siku moja mzazi wa mchezaji mwenzake alileta malalamiko kuwa Zlatan aondolewe katika timu hiyo. Mzazi huyo alilalamika kuwa ana mtoto mmoja tu lakini Zlatan alihatarisha maisha yake. Inasemekana Zlatan alimpiga kichwani kwa makusudi. Siku iliyofuata Zlatani akiwa mazoezini alimuona mchezaji yule anapita na karatasi akiwapa watu wasaini. Hakuelewa chochote.

Jioni yake, kocha alimfuata nyumbani na kumweleza yule kijana amekuja na barua kutoka kwa wazazi wake akitaka ufukuzwe kwenye timu. Malmo FF ilimhitaji sana Zlatan na ilikuwa vigumu wao kupitisha ombi lile. Cha ajabu wala Zlatan hakuomba msamaha.

Kati ya mambo Zlatani asiyopinga ni kwamba alikuwa ni mtu wa hasira kila mara hasa enzi za utoto wake na alijutia sana kwa utukutu wake.

Apata shavu Malmo FF
Alisaini mkataba wake wa kwanza ndani ya Malmo FF akiwa na Miaka 15. Msimu wake wa kwanza mwaka 1999, katika michezo sita ya mwanzo alifunga goli 1 tu. Klabu yake ya Malmo ilimaliza ya 13 kwenye msimamo wa Allsvenskan akiwa na magoli 12 kwenye michezo 26.

Zlatan anasema ilikuwa wakati mgumu sana kwake. Aliona ni mkosi mkubwa sana.

Mchezo dhidi yao na Halmstad ulikuwa mchezo wao muhimu kabisa katika ligi kwani ungeikomboa timu ile kwenye hatari ya kushuka daraja. Morali ya timu ingerudi na ingejenga upya imani kwa mashabiki. Usiku wake hakulala akiwaza kwa namna gani atakavyoiokoa Malmo FF ambayo ni timu yenye mafanikio makubwa zaidi Sweden. Kazi ilikuwa moja tu “kutokushuka daraja msimu wake wa kwanza”. Heshima ya Malmo FF kule nchini Sweden ni sawa na Man United nchini England.

Wakiwa njiani kwenye gari Zlatan hakuongea na mtu yoyote. Walipoingia uwanjani mashabiki walikuwa kinyume nao.

Mashabiki wote walibeba mabango wakituzomea. Nilijuta sana kwanini nimeyachagua maisha haya. Jambo zuri ni kwamba tulianza mchezo kwa kasi ya ajabu, kuwatia moyo mashabiki” Zlatan.

“Nikiwa uwanjani nilijua fika hii ni kwa mara ya kwanza Malmo Inashuka daraja miguu ilikuwa mizito, kila mpira niliogusa nilihisi napiga jiwe maana nilikuwa natetemeka ilikuwa mizito na alikuwa ikitetemeka.”

Mungu sio athumani wakiwa nyuma magoli mawili kwa moja dakika ya 93 Malmo FF walizawadiwa penati. Uwanja mzima ulilipuka. Zlatan akiwa na magoli 12 tayari mashabiki waliamini mfungaji wao bora atakwenda kuwatoa kwenye mdomo wa mamba.

Palitokea sintofaham kwa sababu mwalimu alikuwa amekwisha kumpanga Tony Flygare kama mpiga matuta. Mashabiki walipiga makelele wakimtaka Zlatan akapige tuta.

Unataka kujua kilichotokea basi usikose toleo lijalo.
.
ZLATAN AMKANA RAFIKI YAKE KISA UMAARUFU
.
HATMA YA MALMO KWENYE MKWAJU WA PENATI.

Imeandaliwa na Priva ABIUD 0763370020Read More

Share.

About Author

Comments are closed.