Sunday, August 25

Tunaibeza Welayta Dicha kwa lipi hasa?

0


“Je Tumejirekebisha Kwa Michezo Ya Kimataifa..”

Na *DANIEL S.FUTE*

JUMATANO ya tarehe 21 Machi 2018, zilifanyika droo ya michuano ya CAF kwa vilabu. Moja ilikuwa droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya makundi na nyingine ni droo ya Kombe la Shirikisho katika hatua ya mtoano.

Moja ya vitu ambavyo tulikuwa tunangojea na kushadadia, ni pale ambapo tulipokuwa tunaingojea droo ya Kombe la Shirikisho maana huku ndio tumebaki na mwakilishi mmoja kutoka Tanzania.

Tumebaki na Klabu ya Yanga,huyu ndio mwakilishi pekee aliyebaki. Haijalishi kwamba alishindwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kinachotupa nguvu bado anaendelea kupanda Ndege. Mabadiliko ambayo yamebadilika ni kutoka Mabingwa Afrika kuingia Shirikisho.

Droo ikachezeshwa na hatma ya Yanga ikaangukia mikononi kwa “Wolayta Dicha” ya kutoka Ethiopia. Lakini baada ya droo hii nikajawa na maswali mengi na hayo maswali yalitoka kwa moja kwa moja kwa mashabiki wa Yanga pamoja na watani wao.

Unajau walikuwa wakisema nini, wale wahusika wa klabu yao waliongea kwa jeuri wakisema ‘Sisi hatuwezi kubabaishwa na klabu yenye miaka 18’. Watani wao waka wajia juu na kusema ‘Huyu ndiye aliye mtoa Zamalek,Mnawezaje kuchomoka’?.

Nilishindwa kuwajibu pale maana na wafahamu hawa watani,nikajisemea moyoni nitawajibu kwa maandishi. Swali kubwa ambalo nalipeleka kwa hawa mashabiki wa hizi timu za Kijadi,Je tayari tumejirekebisha na michezo hii ya kimataifa au bado tunaendelea kucheza kwa mazoea? Kwa swali kama hili ni gumu kwao,wanafanya hivi kwaajili ya ushabiki na matambo lazima yaendelee.

*WELAYTA DICHA ILIANZA MWAKA 2009*

Ni timu ambayo inatoka katika ligi ya Ethiopia,na ilianzishwa mwaka 2009 ambapo ilianzia ligi daraja la kwanza mpaka kupanda ligi kuu ya Ethiopia.

Wakati huo wote ilikuwa chini ya mkufunzi Ato Zenebe Fisseha.

*YASHIRIKI MICHUANO YA KIMATAIFA KWA MARA YA KWANZA*

Katika msimu wa 2016-17 Welayta Dicha iliweza kuchukua ubingwa wa Kombe la Ethiopia, ambapo hapo ndipo walipopata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.

Katika mzunguko wa kwanza katika michuano ya kimataifa walipangiwa na timu kutoka Zanzibar Zimamoto,ambapo waliweza kuiondosha kwa idadi ya mabao 2-1 na kusonga hatua nyingine.

*YAITOA ZAMALEK*

Baada ya Zimamoto, ilipangiwa Zamalek lakini kutokana na maandalizi mazuri ya timu yao hawakuweza kutishika na waarabu hao.

Maana katika mchezo wao wa kwanza waliweza kupata ushindi wa 2-1 katika ardhi ya nyumbani, na mchezo wa marejeo wakiwa Cairo walifungwa 2-1 kutokana na faida ya mchezo wao wa kwanza waliweza kwenda hatua ya penati na kuibuka washindi.

*KITU CHA KUJIFUNZA KWA YANGA KUELEKEA MCHEZO HUU*

Kama wangekuwepo na Simba katika michuano hii ingebidi na wao wajifunze hapa,maana hii si kwa Yanga tu ni kwa timu zote kutoka hapa nyumbani kushindwa kutumia game plan katika michuano hii hasa unapoanzia nyumbani.

Ukiitazama michezo miwili ya nyuma,ule dhidi ya Township na Simba dhidi ya Al Masry. Ile michezo tulijimaliza wenyewe katika ardhi yetu kama tungekuwa na game plan ambayo wenzetu huwa wanaitumia wanapokuwa ugenini au nyumbani basi sasa tungekuwa tuna tabasamu kwa mazuri.

Yanga anaenda kukutana na Welayta ambayo imeshinda mechi zote za Shirikiso ikiwa katika ardhi yake ya nyumbani. Lakini pia inakutana na timu ambayo ina uwezo wa kupata goli ikiwa ugenini,maana wamefanya hivyo kwa Zimamoto pale Zanzibar na Zamalek mjini Cairo.

Si fikirii kama safari hii tunaweza tena kurudia makosa,maana umekuwa ndio ugonjwa wetu wa kila nyakati kushindwa kupambana tupokuwa wa kwanza kuanzia katika ardhi ya nyumbani. Yanga inaweza kubadilika watakapo jitambua na kutazama mifano yao wenyewe katika mchezo dhidi ya Township na ule mchezo wa watani wao dhidi ya Al Masry.

Watakapo fanya hivyo na imani kubwa sana watasogea katika hatua sahihi. Tofauti na miaka ya nyuma ambapo huwaga ni kikomo kwetu katika michuano hii ya kimataifa.

Unapoitazama Yanga ambayo ipo nafasi ya pili katika ligi na ukiitazama Wolayta ambayo ipo nafasi ya nane, kuna tofauti kubwa sana lakini tusiibeze sana Welayta maana wenzetu wanatambua game plan ya mashindano haya ya kimataifa tofauti na sisi.

Na katika hatua hii ya mtoano hatma ipo katika michezo miwili tu,ule utakaonzia nyumbani na mwisho ni ule ukiwa ugenini.

Yanga mnahitajika kupambana na kumaliza mchezo, katika hatua hii ya kwanza katika ardhi ya nyumbani. Hatua ya pili tunaenda kufanya kile walicho tufundisha Township na Al Masry.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.