Tuesday, March 19

Sarri anaweza kumfunga Pep

0


Na Robert Komba
Masaa machache yajayo, ulimwenguni wa soka utaenda kushuhudia burudani kubwa pale katika uwanja wa Stamford Bridge ambapo Chelsea ya Maurizio Sarri watawakaribisha Manchester city ya Josep Guardiola. Yamkini wengi wanahisi wamekwisha kuyajua matokeo ya mechi hii, has a ukizingayia Chelsea wamekuwa mwenendo mbovu hapa katika mwezi November wakipoteza mechi mbili za ligi ya ugenini dhidi ya Spurs na Wolverhampton.


Labda kama mechi hii ingechezwa mwishoni kwa mwezi Oktoba, mqwazo ya watu yangekuwa tofauti, na angalau wachache wangewapa Chelsea nafasi ya kupata matokeo.


Kocha Maurizio Sarri anaingia katika mchezo huu huku akiwa akwisha kupoteza mechi 3 kati ya tatu alizokutana na Guardiola katika nyakayi tofauti ikiwemo iliyochezwa Agosti mwaka huu katika ngao ya jamii ambapo Pep aliibuka mshindi kwa magoli mawili kwa sifuri, dhidi ya Chelsea ambayo kimbinu ilikuwa haijakomaa kiasi cha kutosha, na labda mechi hii unaweza kutuonyesha labda nzuri zaidi kwani Chelsea katika miezi minne chini ya Sarri, tayari imekwisha kutuonyesha aina ya mpira inayoelekea kuucheza.

Hivyo kabla ya kuangalia nini Sarri anaweza kukifanya, tuanze kwa kuangalia nadharia ya kiufundi ya Manchester city chini ya Guardiola.

City wanatumia falsafa ya mchezo wa pasi unaoambatana na utumizi wa hali ya juu wa nafasi katika kila hatua ya mchezo kutoka kwenye kuzuia hadi kushambulia hujulikanao kama “positional play” ama “ Juego dé posicion” kwa kihispania.

Pep anauona uwanja kama sehemu iliyogawanyika katika vyumba vitano virefu (sehemu mbili za wazi za nje, nusu nafasi mbili kila sehemu-‘ half spaces’ na eneo la katikati) ambapo sheria kubwa katika mchezo wake kama ulivyoelewa na Mwandishi Marti Pernanau katika kitabu cha Pep Confidential; ni kuwa haitakiei katika wakati wowote wachezaji zaidi ya wawili hawatakiwi kuwa kwenye mstari /chumba kimoja.

Sifa kuu ya kutawala mchezo kwa Man city umekuwa ni utumiaji wa “inverted full backs”, city imetumia mamilioni ya pesa kununua mabeki wa pembeni wenye ubora (Mendy,bDanilo, Walker) kulifanikisha hilo.

Ambapo mabeki hao wa pembeni (isipokuwa Mendy) hutakiwa kuingia sehemu ya kiungo na kufanya city kucheza na wachezaji watatu katika eneo hilo na huku kukiwa na washambuliaji watano nje na ndani ya boksi la wapinzani, huku mawinga (Sane na Sterling) wakiwa pembeni kabisa karibu na chaki kwa ajili ya kutoa mapana ya ushambuliaji yaani Attacking width na kisha kuingia kwenye box kwa haraka. hii inaisaidia city kuepukana na mashambulizi ya kushtukiza kwani hushambulia na wachezaji watano na kuzuia na wachezaji watano, lakini pia umbali kutoka katikati ya uwanja hadi eneo la pembeni ni katibu kuliko eneo la juu ya uwanja hivyo no rahisi kwa mabeki hao kuchukia nafasi zao kwa haraka kuzuia mashambulizi ya wapinzani.

City huwa pamoja katika mda mwingi wa mchezo na hivyo kufanya urahisi wa kuurudisha mpira Mara tu wanapoupoteza kwa kufanya pressing na kukaba kitimu. City wamekuwa wakitawala michezo na kutumia mpira mda mwingi kwa ajili ya kutengeneza nafasi na tayati wamekwisha kufunga magoli 45. katika mechi 15 za ligi msimu huu.

Lakini Chelsea haijawa mbali sana katika kumiliki mpira kwani mtindo wao wa uchezaji unahusisha kupiga Pasi za haraka kutoka nyuma na kukupeleka mpira mbele kwa Pasi za wima (vertical pass) mpaka kwa mshambuliaji wa kati ambaye anafanya combinations na viungo washambuliaji, huku mabeki wa pembeni wakiwa mbele juu kutoa mapana. Kitu ambacho kimekuwa changamoto kwa Chelsea hadi sasa ni kuzuia nafasi ya pembeni has a kushoto wakati wa kushambulia, nafasi ya wazi eneo la mbele ya mabeki wa kati kutokana na kqsi ndogo ya Jorginho na changamoto kubwa ni pale wanapofanyiwa pressing ya mtu kwa mtu katika eneo la kiungo na kushindwa kukupeleka mpira mbele na kufanya mabeki wawe na umiliki mkubwa wa mpira.

Wazo la kumzuia Jorginho hasipate mda mwingi na mpira limetekelezwa na makocha wengi na imeonekana fika jinsi gani baadhi yao ikiwrmo Maurizio Pochetino wamefanikiwa katika hilo. Hivyo hayo ni mambo ya kuyatatua kwa upande Chelsea kabla hata ya kuangalia nini watawafanya city.

NINI CHA KUFANYA
Chelsea watatakiwa kuwaweka mawinga wake eneo la pembeni karibu na chalk ili kuwalazimisha mabeki wa pembeni wakiwa city kuvutika pembeni zaidi na hivyo kuikosesha nguvu timu yao katika eneo la katikati na kisha Chelsea itaweza kupitisha mipira mirefu moja kwa moja katika eneo hilo ambayo itamkuta Giroud mbenye uwezo mkubwa wa kuinasa na kuwaleta wengine mchezoni, city walipata changamoto hii dhidi ya wolves ambapo utumiaji wa mfumo wa 3-4-3 uliwafanya mabeki wa city wafichuliwe kwa kuacha nafasi kubwa nyuma yao pale walipocheza kama inverted fullbacks kwa kuingia katikati ya uwanja.
Pili Chelsea watatakiwa kuwa na kasi zaidi katika kufanya maamuzi ya kukupeleka mpira mbele. Sio kasi ya mchezaji kukimbia na mpira, Bali ni kasi ya mpira kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kitu ambacho pia kimekuwa changamoto kwa Chelsea kwani kasi ndogo ya pasi hufanya wapinzani wajipange na kufanya timu kuwa na umiliki mkubwa wa mpira husioendana na uwiano sawa wa nafasi zilizotengenezwa. Lakini pasi zenye kasi pia ni njia mbadala ya kuweza kupenya mtego wa high pressing ambayo ni silaha kubwa ya man city.

Tatu, ni kuimarisha mpango wa pressing, sio kufanya press kwajili ya kuwachanganya wapinzani Bali kufanya pressing kwa kujipanga katika utaratibu Fulani mzuri , Sarri anaweza kuacha kupress kwa kutumia muundo wa 4-4-2 kama ambavyo amekuwa alifanya lakini badala yake kuongeza idadi katika eneo la mbele kwa kupress na mtindo wa 4-3-3 ambao unaweza kuwapa ugumu zaidi city ambao hufanya ujenzi wa mashambulizi kwa kumtumia golikipa wao hivyo kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu katika eneo hilo (Numerical superiority).

Liverpool wamekuwa wakifanikiwa sana pale wanapocheza na city kwa kulifanya hili, kwani badala kutka kutawala mpira, wao hutawala nafasi na kuizuia hili city ambaye anatawala mpira hasipate nafasi ya kupita.
Kwa njia hizi ambazo yamkini sio kasi rahisi kuzifanikisha zooote kwa usahihi ni wazi kwamba Chelsea wataweza kupata matokeo dhidi ya city na kama sababu zingine za kisaikolojia kama kuanza mechi vibaya kwa Chelsea, na kukosa hali baada ya kuruhusu goli, hazitaiathiri Chelsea basi ni wazi ushindi utakuwa juu yao.

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply