Saturday, August 24

Road 2 Russia; soksi za messi hazinuki tatizo viatu alivyopewa

0


Tiketi ya Bombardier

Ukiachilia mbali taifa la Uingereza ambalo ni taifa lenye mashabiki wenye Viherere sana, kwa mtazamo wangu hapa Afrika Tanzania nasi tumo lakini kwa kule America basi argentine. Timu ya taifa ya Argentine ni moja ya timu nzuri sana lakini imekuwa na migawanyiko mkubwa wa kimtizamo. Sio makocha na sio wachezaji wa zamani ambao wamekuwa na lugha tofauti.

Hivi majuzi zilizuka taarifa kadhaa kuwa Maradona amemlaumu Lionel Messi kuwa sio kiongozi mzuri. Alikuwa amekaa na Pele kwenye droo ya Euro 2016. Pele akamuuliza kama ana ukaribu na Lionel Messi, Maradona akamjibua akamwambia kuwa Messi hana shida ni mtu mtaratibu shida yake hawezi kuongoza watu na amesababisha mgawanyiko mkubwa kwa mashabiki na ndani ya timu.

Wakati wa mazungumzo yale walikuwa wakingong’ongeza bila kujua kama vinasa sauti vilikuwa vimeshawashwa tayari.

maraona na pele

Baadae waandishi wa habari baada ya kuinsasa sauti ile walimfuata pele na kumuuliza kwanini aliamua kumuuliza Maradona swali lile? Pele kidogo alipigwa na butwaa imekuwaje mazungumzo ya watu wawili yamegundulika.

Lakini Pele sio mnafiki aliamua kukisema kile ambacho yeye anaamini. Alisema Messi ni bora na ni mtu wa muhimu katika kikosi hajawahi kuona upungufu wowote kwake.

Anaamini kuwa;

kinachomuangusha Messi sio kwamba ni uongozi wake bali timu nzima inamtaka yeye afanye kila kitu. Ni tofauti kidogo na Brazil ya miaka ya 70 ambapo karibia wachezaji wote walikuwa wazuri na walijituma

Pedro Pasculli yeye ana msimamo kama wa Pele. Mshambuliaji huyu nguli wa zamani wa Argentine amemkosoa Maradona na kusema kuwa Messi anategemewa mara kumi zaidi kuliko Maradona alivyotegemewa 1986. Anakiri kuwa Messi anabeba mzigo ambao Maradona mwenyewe asingeuweza.

Hata kocha wa Zamani wa Argentine Gabriel Batistuta yeye alisimamia msimamo ule ule wa Pasculli. Batistuta anaamini kuwa Maradona ana wivu dhidi ya Messi. Batistuta alikebehi kuwa

kama uongozi ni kuongea ovyo basi ni kweli hana uongozi mzuri, lakini akaongeza kuwa, messi anaweza kuwa na kigugumizi mbele za watu lakini kwenye vyumba vya kubadilishia nguo watu wote huwa wanamsikiliza na anakuwa na ujasiri mzuri tu.

Jorge Barruchaga anaamini Messi hahitajiki kuongoza watu maana yeye sio mwanasiasa, cha muhimu ni yeye kuweza kujiongoza mwenyewe maana na uwezo mkubwa yeye kama yeye na ana uwezo mkubwa wa kubadilisha matokeo.

Nawaza sana kwa namna Argentine hii ambayo ina wachezaji bora duniani. Kufika fainali ni mafanikio makubwa na sio ya kubeza lakini kwanini wanashindwa kukamilisha safari?

Binafsi yangu Messi ni bora mara tatu zaidi ya Maradona. Mafanikio pekee sio ubora wa mchezaji. Leo hii goli moja la mkono linampa Maradona kauli za kishujaa. Kuna mengi sana yamejificha kwenye kivuli cha Messi. Hao viongozi wa uwanjani ambao Maradona anawezema wenye dunia ya soka la sasa hawapo.

Soka la sasa ni uwezo na akili tofauti na soka la hapo awali ambapo jitihada, nguvu, hamasa, kujituma n.k vilitosha kuleta mafanikio makubwa sana kwa baadhi ya timu za taifa. Hao viongozi kwa sasa hawapo. Soka limebadiika mno. Zamani ilikuwa nahodha lazima afoke, aruke tiktaka, atokwe na madamu achafuke mpaka maini na figo sio jezi pekee.

messi na Maradona

Shida nayoiona Kuna wachezaji wamekuwa na misimu mizuri ndani ya vilabu vyao lakini wanakuwa na bahati mbaya ya kutokufunga timu zao za taifa. Kwa mfano Gonzalo Higuan amekuwa na misimu mzuri sana akiwa na Napoli na Juventus. lakini anapokuja suala la timu ya taifa anakuwa tofauti.

Shida ya Higuan sio tu kushindwa kufunga magoli, tatizo ni kwa namna anavyocheza, mvivu, hajitumi, muda mwingi anatembea sana uwanjani. Hajipi kazi sana kwa sababu ana amini Messi yupo.

dybala na Messi

Dybala pia amekuwa akifanya vyema na Juventus lakini tatizo ni nafasi anayocheza. Amekuwa akicheza kama smhambuliaji wa kulia nafasi ambayo Lionel Messi anacheza. Hii inampa waati mgumu sana. Tokea alipopata nafasi ya kucheza timu ya taifa mwaka 2015 chini ya mwalimu Gerardo Martino amecheza michezo 10 tu na hajawahi kufunga goli lolote.

Migogoro isiyoisha

Baada ya kauli tata za baadhi ya wachezaji kama Dybala kwa Lionel Messi zinaonekana kumpa mwalimu Sampaoli wakati mgumu sana kwenye maamuzi. Dybala alisema kuwa anamheshimu sana Messi na anamkubali sana tu, lakini Messi haongeagi nae.

Dybala anasema 

“sijawahi kumkosea, ila mimi na yeye sio marafiki nje ya uwanja na ndani ya uwanja”.

Kama ni wewe kocha wa timu ya taifa kwa kauli hii utakuwa kwenye wakati gani? Wachezaji wako bora hawana mahusiano mazuri?

Tena Dybala anasema haoni tofauti yake yeye na Messi uwanjani na anapambana kila siku kumfikia au kumzidi.

“Sipendi kufananishwa na Messi wala sitaki kuitwa Messi wa baadae, yupo Messi mmoja tu na hakuna mwingine na mimi nitajenga jina langu na ndio lengo langu”

Tayari kuna nafsi zinacheza kushindana uwanjani. Kimsingi mwalimu hapa lazima amtokee kafara Dybala ili kumfaidi Messi. shida kbwa kwa Mauro Icard imekaa kifigisu figisu sana. huenda ni kweli Lionel Messi anahusika. taarifa za chini kwa chini zinadai kuwa rafiki yake  Messi mkubwa ajulikane kama Maxi Lopez.

wanda Nara me wa Zamani wa Maxi Lopez akiwa na Icard

Lopez alipokonywa mpenzi wake ajulikanae kama Wanda Nara na Icard. Lopez alikanusha kuwa kutokujumuishwa kwa Icard hakuhusiki kabisa na tukio hilo. Alisema pia hawezi kumsamehe kabisa Icard na mpenzi wake huyo wa zamani. Lopezi ni rafiki mkubwa wa Maradona.

Baada ya tukio lile Maradona aliongea hadharani kuwa wasaliti hawawezi uitwa timu ya taifa. Inasemekana kitendo cha Icard kumsaliti mchezaji mwenzake na kumchukua mke wake kiliwakera sana Messi na Mascherano ambao inasemekana walishurutisha Iacrd kutokuitwa. 

Lakini Lopez alikanusha kabisa madai hayo nakusema hajawahi kuongea na Messi kwa takribani miaka 10 tokea mwaka 2007 alipokuwa Mallorca. moja ya mambo yaliyomuumiza sana Lopez  ni kitendo cha Icard  kuweka picha ambazo zilimuonesha mwanamama huyo nusu uchi. Lopez alilalamika kuwa zinaleta picha mbaya hasa ka watoto wake. Lopez alisema yeye hana ukarasa wowote kwenye mitandao ya kijamii.

Na anaamini kuwa picha ni siri ya mtu. kitendo cha kuweka picha chafu kama zile zitawathiri watoto wake kisaikolojia hasa ukitazama kuwa yeye ni mtu maarufu. Icard alimuita Lopez mshamba kwa kulalamikia zile picha. bila shaka kitendo hiki kinaweza kuwa sababu kubwa kwa Icard kukosa nafasi timu ya taifa.

Mauro Icard akishangilia bao (nyuma) mbele aliyevaa jezi nyeupe ni Lopez

Lopez alikataa kabisa kushikana mkono na Iacrd walipokutana. ugomvi huu wa Icard na chuki ya chini kwa chini unaweza kuathiri kabisa timu endapo ikiwa kweli Messi anahusika.

 

PATA KIFURUSHI

 

Jina la Utani La Albiceleste

Mfungaji bora; Lionel Messi Magoli 61

Kombe la dunia Mara 2 (1978 & 1986)

Nafasi ya FIFA 5

Michezo mingi Javie Zanetti 145 

 

Tatizo lingine ni uchaguzi wa kikosi

Migogoro na umaaarufu umeathiri kwa kiasi kikubwa ufanisi wa timu ya taifa ya Argentine. Kuna wachezaji hawana haja ya kwenda Russia, sitegemei kuona jina la Javier Mascherano kwenye kikosi ca kwanza, na sina imani sana na kiwango cha Marcos Rojo msimu huu. Rojo anahitajika ufanya kazi ya ziada kujitwalia nafasi. amekuwa na majeruha ya mara kwa mara ambayo yanapunguza ufanisi wake. Bilasha shaka Rojo ni Beki mzuri kiuwezo lakini anahitaji kazi ya ziada.

Rojo anaweza kuitwa lakini suala la kuanza kikosi cha kwanza kwangu bado lina ukakasi. Sidhani kama Rojo atacheza eti kisa tu ni mchezaji wa Man United ila anapaswa kucheza kama atakuwa ameimarisha kiwango chake. timu hazijengwi kwa majina. Hapana timu za taifa hazijengwi kwa mfumo huo. Kinachotazamwa ni ufanisi wake kwa wakati huo na sio uwezo wake kiujumla. Wapo wachezaji ambao wana uwezo na wamekuwa na ufanisi mkubwa msimu huu kucheza nafasi ya beki wa katikati kama vile Nicolas Tagliafico na Nicolas Otamendi.

Wachezaji kama Lautaro Martinez na Cristian Pavon hawapaswi hata kukaa benchi. Nashangaa wanazaa kwenye kikosi cha kwanza huku Paul Dybala na Mauro Icard hawajaitwa au kuachwa benchi. Inawezekana kweli kuna shida kati ya akina Dybala na Icard lakini heshima kubwa ya mwalimu ni kuondoa migogoro binafsi ya wachezaji wake. Ajifunze kupitia kwa Sir alex Ferguson alipomaliza bifu la Cristiano Ronaldo na Wayne Rooney.

Kocha wa Argentine ajiulize sana. Kwanini kukosekana kwa Messi kumezalisha talaka mbili? Talaka ya Kwamba Argentine bila Messi ni uozo lakini watu hawajishia wapo wanasema Argentine ina kocha mbovu. Sampaoli ameonekana mbovu mara baada ya Messi kukosekana tu. Hiki ni kituko. Kama Sampaoli hatomalizana na wachezaji yatamshinda kama Stars ilivyomshinda Maximo.

Maradona ana mchango mkubwa katika kuua soka la Argentine na katika kulikuza. amewekeza muda mwingi katika kukosoa na kuchochea. haisaidii. ninachoamini shida sio bifu la Icard au kiburi cha Dybala au Uongozi wa Messi, shida ni Argentine nzima. kuanzia kocha mpaka Maradona mwenyewe.

imeandaliwa na Priva Abiud

Instagram @privaldinhoRead More

Share.

About Author

Comments are closed.