Sunday, April 21

Ozil “Sijali mimi napiga kazi”

0

Anaitwa Emery Unai. Hana makuu. Hana staa. Yeye anataka kila mchezaji apige kazi. Hapelekeshwi na jina la mchezaji. Akisema amesema. Kilichomponza pale PSG ni kushindwa kuishi na akina Neymar. Amekuja England amekutana na Ozil anayelipwa £350,000 kwa wiki. Ozil ambaye ndiye mchezaji nyota kwenye kikosi hiki.

Amemkuta Ozil soka lake linalekea uzeeni. Ni wakati ambao timu inapaswa kumlinda zaidi kuliko yeye anavyopaswa kuilinda timu yake. Bila shaka Ozil ndiye mchezaji anayetazamwa zaidi klabuni pale. Lakini Unai anajua kilichomzidi pale PSG ni uwezo wake mdogo dhidi ya wachezaji mastaa.

Shida anayokumbana nae kwa sasa ni namna ya kulinda heshima yake kama mwalimu na mwamuzi wa mwisho klabuni.

Uzuri na ubaya wa Ozil ni kipawa chake. Ozil ana kioaji cha hali ya juu lakini kipaji chake pia kinampa kiburi cha kucheza kwa utashi wake kuliko maelekezo ya mwalimu. Mfumo wa Unai wa kucheza kwa kujituma ni kitu ambacho Ozil hawezi kukifanya katika umri wake.

Ubora wa Ozil ni mzigo ambao Unai hataki kuubeba. Makocha wengi duniani huwa wanatengeneza mifumo yao kupitia aina ya wachezaji alio nao bila kuathiri majukumu au uwezo wa mchezaji bora wa klabu. Yaani lazima timu itengenezwe kumzunguka nyota wa klabu. Ndio maana Ole Gunnar ametengeneza timu yake kwa kumzunguka Pogba.

Unai anataka kila mchezaji apambane. Juzi baada ya Ozil kutemwa kikosini, leo ameweka ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter akisema kuwa hatojali chochote ila atapambana. Hii inaashiria kuwa kama Unai hamtaki yeye haondoki. Maanake hana mpango wa kuondoka.

Maana yake nini? Nani atafaulu? Je ni unai atakubali kujenga timu kupitia Ozil au mkeka utamhusu? Je unai akifeli ataondoka mapema kama Mou ata Ozil atauzwa?

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply