Tuesday, March 19

Mourinho kupata sare kwake ni ushindi mkubwa

0


Mchezo kati ya Manchester United, dhidi ya Arsenal, ulikuwa ni mchezo wa kimbinu zaidi kwa timu zote mbili. Mchezo huo uliomalizika kwa mabao 2-2 ulionekana kuwa mgumu sana kwa pande zote, lakini niliamini Mourinho alicheza kamari katika upangaji wake wa kikosi

Aliwaanzisha mabeki watano na viungo wawili wakabaji Matic na Herrera. Aliamini zaidi eneo la kiungo ni gumu sana hasa ukizingatia ubora wa Arsenal. Arsenal wamekuwa na tabia ya kushambulia kwa kupitia pembeni. Jose alijaza mabeki wagumu pembeni na kuweka viungo wakabaji ili kuzina mianya yote ya Arsenal iwe pembeni au katikati.


Hii inatoa taswira Jose, pengine aliamini kama ningeanza na kiungo mchezeshaji asingempa kile anachokitaka yeye uwanjani


Wakati mchezo unaendelea nilimuona Jose, akiwa nje na kuwatupia lawama waamuzi wale wasaidizi wa mezani kwa maana ya kuwatoa mchezoni au kuwajenga kisaikolojia kuwa huu mchezo mkubwa na wenye historia jaribuni kuchezesha haki kwa mtazamo wangu.

Lakini hata ukiangalia kuna faulo zilikuwa zinatokea uwanjani ambazo hata kocha alikuwa apaswi kuwafuata waamuzi ila yeye alijenga mbinu ya kuwatibia kwa maana hata waamuzi watoke mchezoni.

Kama nilivosema hapo awali kuanza mbele kwa Lingard, Rashford, na Martial, kulikuwa inatoa taswira kwamba Jose, anasuburia kushambulia kwa kushtukiza kwa maana ya mpira mirefu.

Wachezaji aliowapanga mbele walikuwa wanakabia juu kwa maana ya kuwafanya mabeki wa Arsenal, wafanye makosa ili kuwaadhibu


Thamini ya vikosi:

🎯Walioanza Man United XI (£209m)
🎽Benchi la Man United (£244.9m)
🎯Walioanza Arsenal XI (£167.9m)
🎽 Benchi la Arsenal(£61.5m)

⚠️Mchezaji aliyeachwa kabisa
Fred (£47m)


Jose Mourinho katika mchezo huu alilenga zaidi kupata sare. Hakukiamini sana kikosi chake. Baadhi ya wachezaji muhimu aliwaweka wazi. Mara kadhaa nimekuwa nikisema Jose, ni kocha mzuri kwenye mechi kubwa ingawa wakati mwingine mambo yanamwendea kombo.


Nyota wa mchezo

Bao la jana la Martial linamfanya kuwa mfungaji bora wa sasa wa United

Michezo: 153 👕
Magoli: 43 ⚽
Dau: £36m 💰

Anthony Martial namba 7 ghali wa Man United wa muda wote.


Arsenal waliumudu mchezo kwani kila mara wao walitangulia kufunga bao na kuwapa United mzigo wa kusawazisha.

Lakini nimejiuliza je kama angetangulia kuongoza je Arsenal, wangerudisha? Sidhani hasa kwa mfumo wa United ingekuwa ngumu sana.

Arsenal waliingia kwenye mchezo huo kwa kuogopa kuwa sisi tuna historia mbovu dhidi ya Utd. Tunacheza kwa hatadhari, pengine lilichangia kupata matokeo haya. Muda mwingi Jose, alikuwa hawalaumu wachezaji wake kwa sababu kile alichowatuma walikuwa wanakifanya.

Makala na Aziz Mtambo

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply