Wednesday, August 21

Morata atemwa, Salah na Ronaldo kuzichapa

0


Rusia watawakaribisha Brazil.
Brazil itakosa huduma za mchezaji wao mahiri kabisa Neymar anayeuguza
majerah aliyoyapata hivi karibuni akiwa na klabu yake ya PSG. Mchezo wa mwisho wa urusi dhdi ya Spain ulitoka sare ya mabao matatu.

Vijana hawa wa Stanislav Chercheov wamekwisha kucheza michezo mitatu huku wakiwa hawajaonja kabisa ladha ya ushindi katika michezo yao ya kirafiki. Mchezo hu utapigwa katika kiwanja cha Olimpiyskiy luzhniki.

Itakuwa wakati muafaka kwa mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firmino kuonesha manjonjo yake kwani msimu huu amekuwa akifunga magoli maridhawa kabisa.

Ureno kuwakaribisha Misri
Mohamed Salah atakutana uso kwa uso na Cristiano Ronaldo kule nchini Uswisi katika kipute hiki cha kukata kwa shoka. Wakali hawa wamewahi kukutana mara kadhaa lakini awamu hii watakutana tena kwenye maandalizi ya kombe la dunia.

Mchezo wa mwisho wa Ureno waliweza kutoka sare ya bao moja kwamoja dhidi ya Marekani ambao wao hawatashiriki kombe la dunia mwaka huu. Katika mchezo huu Ronaldo atarudi tena mara baada ya kuukosa mchezo wa mwisho wa taifa lake. Misri katika michuano ya kufuzu kombe la dunia walifanya vyema sana wakiwa chini ya uangalizi wa Mo sallah anayetamba kule nchini England.

Uhispania kuvutana na Ujeruman
Huu ni mchezo ambao unavuta hisia za mashabiki wengi husasani katika mbara la ulaya.

Ni mahasimu wawili ambao katika makombe mawili ya dunia ya mwisho wamegawana. Mabingwa hawa wa kombe la dunia watakutana kule Espirit Arena kujua nani mbabe. Julen Lopetegui ataendeleza mfumo wake wa kushambulia kwa kasi kujaribu kumfumua Joachim Low. Ni rahisi sana kuamini yeyot atashinda ila ni ngumu kutabiri mshindi. Morata ametemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa baada ya kuwa na msimu mbovu.

Uholanzi dhidi ya England
Mara baada ya viongozi wa juu kabisa wa England kudai kuwa hawatoshiriki kombe la dunia, timu ya taifa itashuka dimbani kufuana na waholanzi walioporomoka kama kiwango cha Mavugo. Ni ajabu sana kusikia eti Italia na Uholanzi hawatakuwepo kombe la dunia. Ni aibu kubwa mno.

Enewei tachane na hayo, Roben hatokuwepo katika mchezo huo. Roben huenda ikawa ni tamati ya soka lake kwa timu ya taifa. Ronald Koeman ameonekana kujali zaidi falsafa za vijana wadogo. Uholanzi wanaingia katika mchezo huu kama mtalii anayeingia kwenye mbuga za wanyama huku akiwa hana silaha yeyote kupambana na samba hawa watatu watakaongozwa na vijana wasumbufu kama Rashford.

Harry Kane bado hatokuwepo baada ya kuumia akiwa na klabu yake ya Tottenham Hotspur

Ufaransa watakichafua dhidi ya Colombia.
James Rodriguez na wenzie watalazimika kusafiri hadi kunako Stade de France kupamabana na Ufaransa. Didier Deschamps ametoa mawazo yake juu ya hali ya Pogba.

Anasema anafahamu kuwa Pogba ana shida na anajua kipi cha kufanya hasa mchezaji wake anapokuwa hana fuaraha. Kiwango cha Antonio Griezman kwa wakati huu utamfanya Didier kukenua tu hasa katika mchezo huu.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.