Sunday, August 25

Mastaa hawa England paliwashinda

0


Luis Alberto (Liverpool 2013-14) – Lazio
Alisajaliwa na klabu ya Liverpool chini ya mkufunzi Brendan Rodgers mwaka 2013. Hakufanya vyema ndani ya kikosi hicho majogoo. Alicheza michezo 9 msimu ule na michezo yote alitokea benchi. Msimu uliofuata jamaa alitupwa nje kwa mikopo mara kwa mara. Maisha yake mapya na klabh yake ya Lazio Msimu yameneemeka mno. Ameassisti magoli 9 na kufunga magoli 8.

Simone Zaza (West Ham 2016-17) – Valencia

Huyu jamaa alituachia kichekesho cha mwaka kwenye michuano ya Euro 2016 kwa kukosa penati kwa staili yake ya mbwembwe. Alipiga penati ya mwendokasi. Mshambuliaji huyu wa kimataifa kutoka Italia maisha yake katika ligi kuu England yalikuwa magumu mno. Magumu sana. Magumu mno mno mno.

Alishindwa kufunga goli katika michezo 11 kitendo kilichofanya mkopo wake kufutiliwa mbali. Kisha alielekea Valencia kwa dili la moja kwa moja katikati ya msimu wa 2016/17. Msimu huu ametikisa nyavu mara 12.

Memphis Depay (Manchester United 2015-17) – Lyon

Boooonge la mchezaji. Noma sana. Ronaldo mpya. Anapiga mikasi kama Dinho, hiyo migoli yake sasa. Huyu ndiye mrithi namba 7 united. Haya yalikuwa maneno ya mashabiki wa United baada ya Depay kusajiliwa mwaka 2015. Alianza kwa mbweeembwee. Mchezo wa pili Old Trafford kwenye michuano ya UEFA akatupia magoli mawili. Kilichofuata baada ya hapo mpaka leo sijui ilikuwaje kwa yule mrithi wa Ronaldo.

Si mnamjua vizuri Jose Mourinho ? Hahaha alimpa michezo 6 tu baada ya hapo akamtoa kwenda Lyon. Huko Lyon sasa. Ana mabalaaa. Waulize PSG aliaapiga Bonge la Goli. Ameonesha kiwango murua sana. Huwezi kuamini ni yule yule aliyetukanwa na mashabiki wa mashetani wekundu. Ndo kwanza ana miaka 24. Muacheni kijana wa Van Gaal msizeeshe na makelele yenu nyie mashabiki wa Old Trafford msio na uvumilivu.

Cristhian Stuani (Middlesbrough 2015-17) – Girona

Jamaa aliwapatia Middlesbrough zawadi ya magoli mawili kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Sunderland. Akawapandisha Mido EPL lakini wakauita flopu akaondoka zake.

Msimu huu ni Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez ndio waliomzidi magoli tu. Jamaa huyu wa Uruguay amewasapraizi sana mashabiki wa Girona kujiweka katika nafasi ya kushiriki Europa League na kujihakikishia nafasi ya kupata nafasi kwenge kombe la dunia.

Iago Aspas (Liverpool 2013-14) – Celta Vigo
Alianzia maisha yake pale Anfield mwaka 2013/14 akiwa na mshambuliaji hatari sana Luis Suarez. Katika michezo 15 alifunga goli moja tu kwenye mchezo wa FA dhidi ya Oldham Athletic. Maisha yake yalikuwa sawa na samaki nchi kavu.

Mpaka sasa ameifungia Celta Vigo, magoli 16 pia akiwa amefunga magoli 111 kwa ujumla akiwa amebakiza magoli mawili kuweka rekodi ya mfungaji bora wa muda wote. Mpaka sasa amifungia hispania magoli matatu kwenye michezo 7 huku akiwa na nafasi nzuri ya kwenda kombe la dunia.

Florian Thauvin (Newcastle 2015-16) – Marseille
Kama kuna mchezaji alibeba vichwa vya habari kwa klabu ya Newcastle basi ni huyu jamaa. Alisajiliwa kwa kitita cha £15m. Kiujumla hakuna alichowafanyia Newcaslte. Hakuwa na msaada wowote zaidi ya kula kulala tu. Msimu huu pale Marseille tayari amefunga magoli 16 na amepata nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa.

Suso (Liverpool 2012-15) – AC Milan

Haka kajamaa kalikuwa bala sana winga ya kushoto. Kakiwa na miaka 18 tu kalimchanganya sana Brendan Rodgers’. Kulia kalikuwepo na haka kajamaa kanaijikunjaga sana mgongo Raheem Sterling aisee walikuwa hatari sana.

Kamwili kake kama ka Juan Mata kalimsumbua sana. Liverpool wakampuuzia. Kakaenda AC Milan, ambapo mpaka sasa ameshacheza michezo 100. Siku hizi hadi namba timu ya taifa anapata. Panga pangua Ac Milan lazima aanze.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.