Sunday, August 25

ligi yetu ndiye chatu anayeimeza taifa Stars

0


Nina mapendekezo yangu kadha wa kadha katika kuinua soka la Tanzania. Kwanza naona tuamshe mwamko mkubwa wa watanzania kulipenda soka lao. Tujenge soka la kesho. Hili la sasa tuwaachie wanaogombania vijiko kwenye sahani ya TFF. Tunahitaji kuangalia shimo la mbele ila sio visiki tulivyojikwaa jana.


Kwanza kizazi cha sasa kipende soka. Nashauri Watoto waingie bure kwenye viwanja vya michezo kama taifa. Nawaona wale wenye matumbo ya njaa watakavyocharuka. Wale mnaowaona wamejaa viwanjani ualaya hawajaanza kwenda viwanjani wakiwa watu wazima, wameanza wakiwa watoto ile ni jadi na ndio maisha yao. je mtoto wa kiafrika tunampa nafasi gani. Inawezekana kuna utaratibu wa watoto kuingia viwanjani.

Lakini hivi majuzi nilikuta watoto wengi wakiwa nje ya geti wengine wakiomba waingie na mimi. Kuna shida. Kuna tatizo hapa. Bora zitengenezwe tiketi za watoto. Bora muweke wazi kuwa mtu akija na mtoto uwanjani apewe ofa. Utahamasisha watu wengi kuja na watoto. Au mnaonaje ? Au kama vipi waingie moja kwa moja

Naam naam.. namaanisha watoto chini ya miaka 17 waingie viwanjani bure au akija na mzazi yule mzazi apunguziwe gharama za kuingia uwanjani, kama tiket 5000 ukija na mtoto ulipe 4000. Mtoto mdogo hafanyi biashara hana chanzo chochote cha kipato, lakini hawa ndio watakao kuwa na uchu wa kutaka timu zao zifanikiwe hapo baadae. Mtoto wa miaka 12 leo akiwa anamuona kichuya uwanjani kesho akiwa na miaka 20 huwezi kumwambia aangalie mpira kwenye TV.

Nimewaza sana kwa namna tutainua soka la sasa nimegundua kuwayang’anya watu vijiko vyao itakuwa kazi. Basi tujenge kizazi cha kesho. Vile viti vya taifa hata msipoingiza watoto bure bado havitawaingizia kitu vitakuwa wazi. Kwa sababu watu hawaendi uwanjani.
Siku hizi si mnarusha mechi laivu? Sikatai mechi zisirushwe, basi angalu fanye ujanja ambao mechi haitarushwa eneo mpira unapochezwa. Maana mkirusha mechi laivu Sasa watu wataenda taifa kufanya nini? Au mkiona nikazi sana basi watoto walipe hata buku au 2000.

Kingine nashauri kuhusu vijana wa Serengeti boys. Mchezaji yoyote atakeingia kwenye kikosi cha timu taifa ya vijana basi lazima serikali impe wakala au mlezi wake kisoka. Namaanisha nini? Naamaanisha serikali itenge kiasi pesa cha kuwapeleka hawa vijana katika akademi za ulaya kwa ajili ya kukuza vipaji vyao na majaribio.

Kwa mfano wakala mmoja apewe vijana wawili apewe jukumu la kuhakikisha akienda nao ulaya asirudi nao. Vipo vlabu vingi vyenye akademi mbali mbali ulaya. Nenda huko Celtic, nenda KRC genk, nenda Malmo FF nenda Sweden huko wakabidhi kijana mmoja au wawili.

Mohammed Belmaachi wakala kutoka Norway aliyekuwa akifuatilia michuano ya AFCON

Waambie wamkuze kijana kwa makubaliano. Musitake wawalipe hapana, ila iwe jukumu la serikali kumpa kijana huyo posho. Huyo kijana akikaa miaka miwili akija hapa atakuwa na uwezo mkubwa kuliko baadhi ya vishoia wa hapa ligi kuu. Baada ya miaka kadhaa wakirudi wanarudi wakiwa na miaka 21 mpaka 23 nina hakika hawatokosa timu za kucheza huko ulaya. Tusitegemee timu ya taifa inayotokana na Simba na Yanga. Tusitegemee soka Bora kutoka kwa Simba na Yanga. Ni maigizo haya. Wala haiwezi kutokea. Haipo hiyo.

Hata Brazil wenyewe hawategemei wachezaji wa timu ya taifa watoke ndani ya ligi zao. Ni ngumu mataifa masikini kutegemea wachezaji wao wa ndani kufanya vyema. Mantiki ya kupeleka wachezaj ulaya ni kutangaza jina la Tanzania. Leo hii ukiwa na vijana 10 ulaya utashangaa maskauti wa akina Arsen Wenger wanakuja huku.

Unaweza ukaona michezo haina faida lakini naomba nikwambie kitu Brazil ina wachezaji milioni 2.1 waliokwisha sajiliwa pote duniani. Brazil ina vilabu 29,208. Kila klabu ina uwezo wa kubeba vijana 30.

Tanzania tuna vilabu visivyopungua 1000, kila klabu iliyopo ligi kuu na ligi daraja la kwanza ina uwezo wa kuwa na wachezaji sio chini ya 30. Kimahesabu hapa tuna uwezo wa kuajiri wachezaji 1000.

Kati ya hao 1000 wacheaji 200 wanaweza wakawa wanalipwa mshahara usiopungua laki 5, kila mchezaji hapa ana weza kuajiri watu wasiopungua watano wakala, meneja, mshauri, daktari binafsi, vijana wake wa camera n.k, na wakili wake. Kila aliyeajiriwa na mchezaji huyu ana watu watatu au watano wanaomtegemea. Kila mchezaji nae ana watu sio chini ya watano wanamtegemea yaani nazungumzia familia. Je hapa hujapunguza ufukara wa watu million? Je waandshi wa habari hawatafaidika kwa hili?

Soka lina nafasi kubwa sana kwa vijana ambao hawana ajira lakini wamejaliwa vipaji. Soka linaweza kuokoa maisha ya familia milioni. Faida ni kubwa kwa sababu serikali haitatumia gharama za moja ka moja ila mzunguko wa fedha utarudi pale pale.

Mashabiki watajaa viwanjani, wachezaji watalipa kodi na vyombo vya habari vitachangia. Kwanini tusijenge misingi imara katika wizara ya michezo?

Kwa mfano Brazil hapo awali ilikuwa na wizara ya michezo na utalii lakini baadae wakaziteganisha. Angalia namna soka lilivyoondoa umasikini Brazil? Leo hii ukipiga kampeni za kisiasa brazil usipoelezea utaifanyia nini soka huna lako. Natamani hata tungekuwa na wizara tofauti. soka letu ni dogo lakini lina faia kubwa kiasi kwamba hatupaswi kuimezesha na wizara nyingine. Wizara hii ya inayoshughulika na michezo ni kubwa mno.

Kwa mfano tu, kwenye burudani kuna muziki, kuna filamu, kuna masuala ya utamaduni kama ngoma, kuna fasheni, kuna sanaa mbalimbali, kuna suala la mashindano ya mamis nakadhalika. Kwa upande wa michezo kuna michezo mingi sana mathalani kila mtu anajua. Kuna TFF, BMT, sjui chaneta, sjui kuogelea n.k. hii ndio sababu kubwa baadhi ya michezo/sanaa kufa kwa sababu, baadhi tu inapewa kipaumbele zaidi. Wizara ya michezo iwe kivyake, na wizara ya utamaduni na burudani isimame kivyake.

Imeandaliwa na Priva ABIUD 0763370020

Waweza nifollow Instagram kwa Privaldinho.

Usiache kusbscribe youtube Channel ya Dauda Tv.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.