Monday, March 18

EPL inazidi kuongeza kachumbali

0


Na Robert Komba


Mwandishi wa kitabu cha soka “The mixer” kinachoelezea historia na maendeleo ya mbinu za soka katika EPL, Anaitaja ligi hiyo kuwa ni “mixer” yaani mchanganyiko wa mbinu mbali mbali za soka. Akiwataja makocha kama Pep Guardiola, Antonio Conte, Jurgen Klopp, Jose Mourinho na Mauricio Pochetino kwa jinsi wanavyoonyesha mchanganyiko wa mbinu katika ligi hiyo.


Yamkini alikuwa sahihi alipoandika kitabu hicho januari ya mwaka 2017,kwani mwaka 2018 tumeshuhudia ujio wa makocha Maurizio Sarri, Unai Emery na Nuno Espírito Santo.


Uwepo wa makocha wenye falsafa tofauti za soka unaifanya ligi ya uingereza kuvutia zaidi, kwani mechi nyingi za ligi zinatoa uhondo kwa kuangalia nani ataziweza mbinu za mwenzake.

Na kwa upande wa makocha wanapata kukabiliana na mbinu tofauti na kwa namna hiyo wanaboresha mbinu zao. Kufundisha katika ligi ya Uingereza kwa sasa inampa kocha changamoto inayofanana na ile wanayoweza kuipata wakiwa katika ligi ya mabingwa kwani wanakabiriana mbinu tofauti.

Hivi Leo klabu ya Southampton imetangaza kumwajili kocha Ralph Hasenhüttl ambaye ni imani yangu anakuja kuinogesha zaidi ligi hiyo.

Kocha huyo anajulikana kama “Jurgen Klopp wa Austria” kwa kuwa wanafanana sana kwa falsafa na mjerumani huyo. Falsafa ya kukabia juu kwa mtindo wa namna yake (Geggenpressing).


Ralph alishawahi kunukuliwa akisema

Klopp ni rafiki yangu,tunajuana sana na tulifanya kozi zetu za ukocha pamoja”.


Ralph ameshafundisha timu kadhaa hadi sasa, lakini amepata mafanikio zaidi katika Klabu ya RB Leizipig ya ujerumani ambapo katika msimu wa 2016/17 aliifikisha nafasi ya 2 nyuma ya Bayern Munich.

Aliweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kufanya hivyo katika msimu wa kwanza. Lakini kilichovutia zaidi ni mtindo wa pressing na mfumo wa 4-2-2-2.

Timu alizofundisha Ralph

LEIZPIG
Msimu wa 2016/17 Ralph akiachiwa timu na aliyekuwa kocha wa Leizipig (ambaye pia ni kocha wa sasa) Ralf Rangnick, alipendelea kutumia mfumo wa 4-2-2-2.

Muhimili wa mtindo wake ulikuwa ni Pressing ambapo aliilekeza timu yake kucheza juu na kubuni mbinu tofauti tofauti kuwazuia wapinzani wasifanye ujenzi wa mashambulizi kutokea nyuma na kujitafutia nafasi za magoli kwa kupora mipira kutoka kwa wapinzani.

RALPH alikuwa na ubunifu kwa viungo wawili washambuliaji (Mdanishi mwenye asili ya Tanzania) Yusuph Poulsen na Forsberg ambapo waliingia katikati ya mistari ya wazi (half space) na kufanya ubunifu kwa kuwatenengenezea magoli washambuliaji Timo Werner na Augustin.

Katika kiungo cha chini kulikuwa na Sabitzer ambaye alicheza kama box to box akizunguka huku na huko kupora na kukokota mipira kuelekea mbele na kumwacha Diego Demme kama namba 6 (ambaye pia alitumiaka kama beki wa kati).

Kimsingi ilikuwa ni timu ya kuvutia,vijana wenye kasi na ubunifu wa kutosha katika mfumo wa kufurahisha na ni matuamini yangu kwamba Ralph anakuja kuibadili Southampton kwa kiasi kikubwa, huku viungo, Mario Lemina, Hogjberg wakicheza chini na Redmond pamoja na Armstrong wakitumika sehemu ya ubunifu kutokea pembeni na kuingia katikati.

Utegemezi wa Kutumia washambuliaji wawili ulioachwa na Mark Hughes unaweza kuendelezwa na Ralph kwani uwepo wa washambuliaji Manolo Gabbiadini, Charlie Austin, Danny Ings na Shane Long utampa Ralph upana mzuri wa uchaguzi katika eneo hilo.

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply