Friday, April 19

Chelsea yamtengea fowadi milion £50

0

“This is Real Man United” hiyo ni kauli ya David De Gea. David De gea kufika sasa amecheza michezo 342 amezuia lango lake kufungwa goli michezo 125.

Magolikipa waliofanya Save nyingi msimu huu 2017/18 :

🥇 D. De Gea — Man United vs Arsenal (14)
🥈 W. Hennessey — Crystal Palace vs Liverpool (12)
🥉 D. De Gea — Man United vs Tottenham (11)

Ramsey amesafiri kwenda Juventus kufanya vipimo vya afya. Ramsey atajiunga na Juventus bure ifikapo mwisho wa msimu


Mara baada ya Fabregas kutua Monaco mchezo wake wa kwanza aliisaidia timu yake kupata alama 1 wakiwa ugenini dhidi ya Marseille. Klabu yake pia ipo mbioni kunasa huduma za fowadi wa Chelsea Mitchy Batshuayi


Mousa Dembele amesafiri kwenda Hong Kong kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya kujiunga na Beijing Guoan


Martin O’Neil anatarajia kuwa kocha mkuuwa klabu ya Nottingham Forest.


Chelsea wanajiandaa kutoa kitita cha Paundi milioni 50 kumnasa fowadi wa Bournemouth Collum Wilson. Lakini klabu hiyo imesema kama Chelsea wanamtaka Collum watoe Paundi milioni 75.


Philippe Coutinho amesema hana mpango wa kuondoka klabuni Barcelona. Kulikuwepo na taarifa kuwa Nyota huyo wa kibrazil huenda akatimka klabuni hapo.


Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply