Friday, August 23

Abdi Banda Mwamba wa Chuma usiotingishwa na kutu

0

::
📅Tarehe kama ya leo Abdi Banda “Mwamba wa Chuma” alizaliwa. Ni mmoja kati ya mabeki wenye uwezo wa hali ya juu. Katika mambo makubwa aliyojaliwa ni uwezo wake wa kucheza nafasi tofauti uwanjani. Ana uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto, beki wa kati na hata kiungo mkabaji. kabla ya yote heri ya mwaka mpya mwamba.
::
📈Katika ligi ya Afrika Kusini kicha ya Abdi Banda kucheza mechi chache ndiye beki namba 5 aliyesafisha mashambulizi hatari zaidi akiwa na wastani wa kufanya hivyo mara 15 kila mchezo huku akiwa amecheza mechi 13 pekee.
::
📉Aina yake ya uchezaji na umbo lake kwa mbali unaweza ukaona miondoko ya Virgil Van Djik wa Liverpool. Van Djik amekuwa na wastani mkubwa wa kuondosha mipira ya kichwa kutokaba na Umbile lake, huku Abdi Banda akishilikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu katika ligi ya Afrika Kusini, ambaye ameondosha mipira ya juu kwa asilimia 70.
::
📊Abdi Banda huyo kumbuka anasumbuliwa sana na majeraha. Msimu wake wa kwanza alicheza mechi 28 na kufunfa mabao matatu, msimu huu mechi 13 na kufunga bao 1
2019: ⚽ vs Black Leopard (1 – 2)
2017: ⚽ vs Orlando Pirates ( 1 – 1) Mechi yake ya 2 ligi kuu tokwa asajiliwe.
2017: ⚽⚽ vs Bloemfontein (2 -2 )
::
🥾NJE YA SOKA: Mbali na soka Abdi ni mchezaji nadhifu sana ambaye inasemekana anaweza kuwa miongoni mwa nyota watano wanaotupia pamba kali sana. Banda ni shemeji wa mwanamuziki nguli nchin hapa Ali Kiba.
::
💰THAMANI: Thamani ya Banda inakadiriwa kuwa yeye ni mchezaji wa tatu kwa thamani hapa bongo. Banda beki mwenye thamani kubwa sana Tanzania ikikadiriwa kufikia Shilingi bilion 2, thamani hiyo inamfanya kuwa beki mwneye thamani kubwa Afrika Mashariki. Katika kikosi cha Baroka Banda ndiye mchezaji wa pili mwenye thamani kubwa.
::
🔋MAENDELEO YAKE: Huu ni msimu wake wa pili katika kikosi cha Baroka na tayari amekwisha kuaminika kiasi cha kukaimu mara kadhaa kitambaa cha unahodha.
::
⚠️KWANINI HAJACHEZA SANA: Msimu huu mambo yake hayajaenda sawa mara baada ya kupatwa majeraha akiwa na kikosi cha timu ya taifa mwezi novemba mwaka jana, lakini pia alilazimika kukaa nje miezi mitatu baada ya kuumia nyonga mwezi wa 1 mwaka huu.
::

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply