Monday, August 19

Mtoto hachezi: Wakati gani umuone daktari?

0


Hili ni swali ambalo  wajawazito wengi  wamekuwa  wakiuliza.  Mtoto kucheza  ni  hisia  za pekee  sana wanazohisi kina mama wajawazito.  Mtoto  anapocheza inamaanisha kwamba mtoto yuko na afya njema
Je mtoto anaanza kucheza lini?
Iwapo mimba  ni ya kwanza kwa kawaida  mtoto  anaanza kucheza wakati wa wiki ya 20. Na iwapo Ujauzito ni wa pili mtoto anaanza kucheza kuanzia wiki ya 16. Hata hivyo mtoto anaweza  kuwahi kucheza  au kuchelewa  kucheza kwa wiki kadhaa  kwa baadhi ya wanawake.  Kama mtoto wako hajaanza kucheza  katika kipindi hicho huitaji kuwa na hofu sana. 
Mama anasikiaje mtoto anapoanza kucheza?
Mtoto anapoanza kucheza mama huisi kama vitu vinamgusagusa tumboni.  Mwanzoni mama anaweza kuihisi kama vile tumbo linajaa gesi au njaa. 
Mtoto  anaweza kucheza mara chache tena bila mpangilio maalumu  katika  muhura  
Ni kawaida  katika  muhura wa pili wa pili wa Ujauzito.  Muda unavyosonga  utamsikia mwanao anacheza kwa nguvu na kila  mara. Unaweza  kuhisi mtoto anavyocheza  kwa kuweka  mkono wako tumboni. 
Kadri  mimba yako inavyozidi kukua ndivyo utakavyokuwa unafamu jinsi  mwanao anavyocheza. Kila mtoto ana namna yake ya kucheza.Watoto wengi hucheza sana kati ya wiki ya 27 na 32. Baada ya hapo huchezaji wa mtoto  hupungua. 
Wakati gani umuone daktari.
Iwapo utagundua mwanao amepungua kucheza au hachezi  kabisa  katika kipindi cha masaa 24 nenda katika  kituo cha afya cha karibu. Hali hiyo inaweza kuashiria kuwa mwanao yuko katika  matatizo.  
#Je Una swali au maoni..cheki kwenye  comments hapo chini
#Share  na mtag mama k yeyote apate  elimu hii..Read More

Share.

About Author

Comments are closed.