Monday, August 19

Je unapaswa kufanya ultrasound mara ngapi wakati wa ujauzito?

0


Ultrasound  ni kipimo ambacho mama mjamzito anaweza kuambiwa kufanya ili kuona maendeleo ya Ujauzito wake.  Kwa kawaida  wajawazito  wengi hufanya kipimo  hiki mara mbili. Hata hivyo ultrasound inaweza kufanya  mara nyingi  zaidi  iwapo kutakuwa na sababu za kufanya  hivyo mfano iwapo  una mimba hatarishi utahitaj kufanya  ultrasound  mara  nyingi zaidi.
Ultrasound  inafanywa ili kuweza kubaini ukubwa na mlalo wa mtoto, kujua mahala lilipo kondo la nyuma, pamoja na  mambo mengine. 
Je unapaswa kufanya  ultrasound mara ngapi wakati wa ujauzito?
Kwa kawaida  ultrasound  inafanywa katika  vipindi vifuatavyo vya Ujauzito:-
Wiki 7-9 : Madaktari wengi hupendelea mama kufanya ultrasound wakati huu wa ujauzito.  Daktari anaweza kuomba ufanye ultrasound katika kipindi hiki iwapo kuna hatari ya ujauzito kutoka, kuthibitisha umri  wa mimba, kuona iwapo mama  ana mapacha, pia kutambua iwapo  mimba imetunga nje ya  mfuko wa uzazi nk.
Wiki 10 -14 : Inafanyika ili kuweza  kubaini iwapo  mtoto ana kasoro za kimaumbile  mfano  magonjwa ya  Moyo na maradhi ya mtindio wa ubongo. Sio rahisi  kufanyiwa kipimo hiki katika maeneo mengi.
Wiki 18- 20: Ultrasound  inafanywa ili kuthibitisha umri wa mimba, kubaini mkao wa mtoto, kupima  ukubwa wa mtoto, kuona kama kuna mtoto zaidi ya mmoja,  kuona iwapo kondo la nyuma liko sehemu  sahihi au hapana, kuona wingi wa maji kwenye mfuko wa mtoto, kubaini kasoro za kimaumbile na kujua jinsia ya mtoto.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.