Wednesday, August 21

Standard Chartered wachangia 1.1% ya GDP ya Tanzania

0


 Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel (katikati) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Makampuni na Taasisi za Fedha wa benki ya Standard Chartered, Jaffer Machano (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Kutoka kushoto ni Mwandishi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii, Rene Kim, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Standard Chartered nchini Tanzania, Ruth Zaipuna, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk. Bernard Kibesse pamoja na Mmoja wa wajumbewa bodi ya benki ya Standard Chartered nchini, Harish Bhatt (wa pili kulia).
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk. Bernard Kibesse (kushoto) akibadilishana mawazo na Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel (katikati) pamoja na Mmoja wa wajumbewa bodi ya benki ya Standard Chartered nchini, Harish Bhatt (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel akifurahi jambo na na Mmoja wa wajumbewa bodi ya benki ya Standard Chartered nchini, Harish Bhatt wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Meza kuu kutoka kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk. Bernard Kibesse, mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Standard Chartered nchini Tanzania, Ruth Zaipuna pamoja na Mwandishi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini, Rene Kim.
 Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk. Bernard Kibesse akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Standard Chartered nchini Tanzania, Ruth Zaipuna akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel (kushoto) kuzindua rasmi ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwandishi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini, Rene Kim akifanya mchanganuo wa ripoti hiyo kabla ya kuzinduliwa kwa ripoti hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wajumbewa bodi ya benki ya Standard Chartered nchini, Harish Bhatt (kushoto) pamoja na Mkuu wa Makampuni na Taasisi za Fedha wa benki ya Standard Chartered, Jaffer Machano wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia), Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk. Bernard Kibesse pamoja na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Standard Chartered nchini Tanzania, Ruth Zaipuna wakizindua rasmi ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Makampuni na Taasisi za Fedha wa benki ya Standard Chartered, Jaffer Machano (kulia) na kushoto ni Mmoja wa wajumbewa bodi ya benki ya Standard Chartered nchini, Harish Bhatt.
 Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia), Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk. Bernard Kibesse(wa pili kushoto), Mmoja wa wajumbewa bodi ya benki ya Standard Chartered nchini, Harish Bhatt (kushoto),  Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Standard Chartered nchini Tanzania, Ruth Zaipuna (wa tatu kulia) pamoja na Mkuu wa Makampuni na Taasisi za Fedha wa benki ya Standard Chartered, Jaffer Machano (kulia) wakipiga makofi baada ya kuzinduliwa rasmi ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa wa benki ya Standard Chartered waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki hiyo kwa uchumi na jamii nchini, iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wateja wa benki ya Standard Chartered, wafanyakazi wa benki hiyo, wanahabari pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki hiyo kwa uchumi na jamii nchini, iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) akizungumza jambo na mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel (kulia)alipokuwa akijiandaa kuondoka ukumbini hapo. Wengine ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk. Bernard Kibesse(wa pili kulia)pamoja na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Standard Chartered nchini Tanzania, Ruth Zaipuna.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na meza kuu mara baada ya kuzindua ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki ya Standard Chartered kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.













Standard Chartered wachangia 1.1% ya GDP ya Tanzania

Na Mwandishi wetu

BENKI ya Standard Chartered imechangia asilimia 1.1 ya pato la taifa (GDP) sawa na kuwezesha huduma na bidhaa zenye thamani ya dola milioni 579.

Taarifa hiyo imetolewa wakati wa uzinduzi wa ripoti ya athari chanya ya mchango wa benki hiyo kwa uchumi na jamii nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena.

Alisema mchango wake pamoja na kusaidia upatikanaji wa kazi, biashara na ukuaji wa uchumi, imekuwa ikichangia maendeleo ya ukuaji wa sekta ya fedha katika miundombinu na utaalamu.

Katika uzinduzi huo uliofanywa na Katibu Mkuu Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel, Benki hiyo imesema kwamba imewezesha nafasi za kazi za moja kwa moja na za msaada zipatazo 220,000 ikiwa ni sawa na asilimia moja ya watanzania wote walioajiriwa.

Kuhusiana na mchango wake katika uchumi wa Tanzania, ripoti inaonesha kwamba Standard Chartered Bank inahusika na ukuaji wa sekta ya biashara kwa asilimia 3.5 na katika viwanda ikiwa ni asilimia 3.7.

Pamoja na kutoa takwimu za mchango wake katika uchumi wa Tanzania, pia ripoti hiyo imeonesha namna bora ambapo benki inaweza kukuza mchango wake katika uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Benki imeshauri kufanya mambo kadhaa ikiwamo kuongeza shughuli zake za kuchochea ukuaji wa biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na kujiimarisha katika soko hilo.

Kuelekeza nguvu zake katika sekta ya uzalishaji bidhaa kwa kusaidia kampuni za ndani kusonga mbele katika uzalishaji wa bidhaa na hivyo kuongeza kasi ya ukuaji wa kiuchumi.

Aidha imeelezwa benki hiyo ina fursa bado za kusaidia watu maskini, ambao ni lazima kuwasaidia kukua kimapato na hivyo kukuza uchumi. Kwa kukua kwa kipato chao Benki itaongeza idadi ya watu wanaotakiwa kuwa wateja wao hapo baadae.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo nchini Tanzania, Ruth Zaipuna, amesema kwamba ripoti hiyo imeonesha mchango wa benki ukuaji wa kiuchumi na hasa sekta binafsi ambayo ndio inatoa wateja.

Alisema benki hiyo itaendelea kufanya juhudi za kuimarisha ushirikiano wake na mataifa ya Afrika Mashariki kupitia bidhaa zake mbalimbali.

Naye  Prof. Elisante Ole Gabriel ameipongeza benki hiyo kwa juhudi zake na kusema  wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano ili kuiwezesha benki hiyo kutoa mchango wake kuimarisha uwekezaji na biashara nchini.

Katika hotuba yake Katibu huyo amezitaka benki nchini kupunguza riba katika mikopo yao ili wananchi wengi waweze kuchukua mikopo na kuwa na uwezo wa kuirejesha.

Aidha kwa kupunguza riba watu wengi zaidi wataenda kuchukua fedha na hivyo kuimarisha mzunguko wa fedha

Prof Elisante Ole Gabriel alizitaka benki zote ikiwemo Standard kutoa mikopo kwa makundi ya vijana na wafanyabiashara wengine bila riba na kutumia fedha wanazorejesha kwa ajili ya jamii kulipia riba.

Naye Naibu Gavana Benki Kuu, Dk Bernard Kibessa, ameipongeza benki hiyo kwa kujifanyia tathmini kuhusiana na shughuli zake nchini Tanzania. Alisema Benki kuu kama mdhibiti wa shughuli za kifedha nchini itaendelea kutoa ushirikiano wake.

Ripoti ya leo ni ya tano ya benki hiyo baada ya nyingine kufanyika nchini Ghana, Indonesia na Bangladesh na ripioti ya Kusini mwa Jangwa la Sahara iliyotolewa miaka ya karibuni.

Standard Chartered imekuwa na uhusiano wa Afrika wa miaka 150 ina zaidi ya matawi 180 na wafanyakazi 8000 katika nchi 15 Kusini mwa Jangwa la Sahara zikiwamo Angola, Botswana, Cameroon, Cote d’Ivoire, Ghana, Kenya, Mauritius, Nigeria, Sierra Leone, Afrika Kusini, Tanzania, Gambia, Uganda, Zambia, na Zimbabwe.



Read More

Share.

About Author

Comments are closed.