Thursday, August 22

SNURA MUSHI KUVUNJA UKIMYA APRILI 2 MWAKA HUU, MENEJA WAKE AWEKA HADHARANI KILA KITU

0


Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
SWALI ambalo mashabiki wa msanii na mwigizaji wa filamu nchini Snura Mushi kama atatoa wimbo mpya au filamu ,jibu swali kupatikana Aprili mwaka huu.

Kwa muda mrefu mashabiki wa muziki na Watanzania wamekuwa wakiuliza kupitia mitandano ya kijamii ni lini Snura atavunja ukimya kwa kuja na kituo.

Akizungumza leo Dar es Salaam,Menaja wa Snura,anayejulikana kwa jina la Hemed Kavu a.k.a amesema swali hilo ni fumbo kubwa.

Hata hivyo amesema Aprili mwaka huu Snura atakuja na ujio mpya katika medani ya muziki pendwa wa Bongo Fleva.

“Matarajio yetu ni kwamba Snura Aprili mwaka huu atavunja ukimya kwa kuweka wazi kuhusu swali hill lenye hastah ya Vumbi LA mguu,” amesema HK.

Uwezo,kipaji, kukata nyonga,sauti na mvuto wa Snura umemfanya kuwa na umaaarufu wake katika medani ya muziki wa kizazi kipya na filamu za kibongo kwa ujumla.

Hivyo kwa sasa mashabiki wanasubiri kwa hamu kubwa kuona nini ambacho mwanamuziki huyo amekiandaa kwa ajili yao maana hajawahi kukosea.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.