Thursday, August 22

Dayna Nyange afunguka kuhusu mwanaume aliyempa ujauzito

0


Baada ya ‘kelele’ kuwa nyingi kutoka kwa mashabiki wa muziki juu ya ujauzito wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Dayna Nyange, hatimaye mwanadada huyo amefunguka, akisema muda si mrefu atamuweka hadharani baba wa mtoto mtarajiwa.
Dyna amekuwa kimya muda mrefu kabla ya kuibuka hivi karibuni na wimbo wake mpya wa Sale Sale unaoendelea kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali za muziki.
Baada ya kuonekana na hali hiyo, mashabiki wake walitaka kumjua baba kijacho wake na hatimaye mwanadada huyo alifunguka na kusema muda si mrefu kuanzia sasa atamuweka wazi mzazi mwenzake hivyo mashabiki watulie.
“muda siyo mrefu ninakwenda kumtambulisha baba kijacho wangu, nakwenda kufanya hili kwa sababu watu wanaonekana wana kiu sana ya kumfahamu kiasi kwamba wanakuwa wanabashiri mpaka kuwagusa wasionihusu kabisa,” alisema dayna.
Dayna alisema kuwa watu wanaobashiri mara kwa mara juu ya baba wa kijacho wake ni kwa sababu wana hamu ya kufahamu na kiu yao anakwenda kuikata hivi karibuni.
Alipoulizwa ni lini hasa anakwenda kufanya hivyo, alisema hawezi kuweka wazi kwa sasa na itakuwa ni jambo la kuwashtukiza watu, lakini ni katika kipindi kifupi kuanzia sasa.
Kama bado hujaitazama video ya Dayna – Sale Sale bofya hapa chihi kuitazama.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.