Saturday, August 24

YANGA FC, TOWNSHIP ROLLERS YA BOTSWANA KUKUTANA

0


Na Agnes Francis, Blogu ya Jamii. 

MABINGWA watetezi  Tanzania Bara Yanga SC wamefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya klabu Bingwa Barani Afrika ambapo watakutana na  Township Rollers kutoka nchini Botswana.
Ambapo mchezo huo utapigwa  katika Dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam  kabla ya marudiano huko kwao. 

Hatua hiyo ni baada ya kulazimisha sare  ya bao 1-1 dhiidi ya St Louis  ya  Shelisheli Katika mchezo  wa marudiano uliopigwa katika  dimba la Stade Linite  kisiwani hapo. 

Ibrahimu Ajibu ndiye aliyeipatia timu ya Yanga SC  bao la kuongoza dakika ya 45+ baada ya kupokea pasi mujarabu kutoka kwa Hassan Kessy upande wa kulia na kuwainua kwa shangwe mashabiki na wapenzi wa timu hiyo, hata hivyo Bernard Esther  aliisawazishia timu yake dakika ya 93.

Mabingwa hao wa soka Tanzania Bara wamefuzu kwa ushindi wa  jumla ya mabao 2-1 ambapo walishinda bao 1-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliorindima Uwanja  wa Taifa Jijini Dar es salaam. 

Endapo Yanga SC itafanikiwa kumtoa mpinzani wake Township Rollers ya kutoka huko Nchini Botwasana itainga hatua ya makundi, lakini kama itashindwa basi itacheza raundi ya pili michuano ya shirikisho inayoshiriki klabu  ya wekundu wa Msimbazi SimbaSc.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.