Sunday, August 18

WIZARA YA AFYA IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII YAANZA KAZI RASMI MJI WA SERIKALI

0


Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imeanza rasmi kutoa
huduma za Ofisi katika mji wa Serikali uliopo Mtumba nje kidogo ya
Jiji la Dodoma na kuwataka wananchi kufuata huduma za kiofisi katika
ofisi hizo mpya. .

atibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John
Jingu amesema kimsingi Ofisi yake kwa sasa inatoa huduma zake katika
ofisi zake zilizoko Mtumba na kuwataka wateja wake kufuata huduma hapo
ambazo zitakuwa wazi muda wote

“Nawakaribisha sana wananchi wote kuanza kutumia ofisi zetu hapa eneo
la Mtumba na tuko hapa kama hatua muhimu ya kutekeleza kikamilifu
agizo la Rais kwa vitendo.” Aliongeza Dkt.Jingu.
.

Aidha, Mkurugenzi wa Utawala na Wizara na Rasilimali Watu Leornad
Mchau amesema ni uamuzi muhimu sana wa kuweka Ofisi za Serikali mahali
pamoja ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwa haraka na kwa
gharama nafuu. .

Ameusifu uamuzi wa Serikali kuwa wa msingi sana akitofautisha na Dar
es Salaam ambapo Wizara za Serikali zilitapakaa maeneo mbalimbali ya
Jiji lakini kwa sasa hata kama ukitokea Jijini Dar es Salaam ni rahisi
kupata huduma za Serikali katika eneo moja.

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya
Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza ametoa rai kwa
uongozi wa Jiji la Dodoma kuharakisha miundombinu ya usafiri ili
wananchi wanaoitaji huduma za kiofisi waweze kufika katika eneo la
Mtumba na kupata huduma hiyo kwa haraka.

Magwiza ameongeza kuwa kwa maoni yake wateja watu wanahitaji
miundombinu rafiki ili waweze kuhudumiwa na ofisi yake kwa haraka
lakini ana imani uongozi wa Jiji utaharakisha au kulifanyia kazi jambo
hili na kuwezesha wananchi kupata huduma ya haraka na kuwataka kuweka
tayari mipango miji ili wawekezaji waweze kuwekeza jilani na eneo
hilo.

Wizara za Serikali tayari zimeanza kutolewa katika Jiji jipya la
Serikali kufuatia agizo la Mhe. Rais la kuwataka Viongozi wa Setikali
kuanza kutoa huduma zao Mtumba baada ya kukamilika kwa Ofisi hizo.

 Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
akifurahia jambo mara baada kuanza kazi Makao Makuu Mapya ya Wizara yake
yaliyoko eneo la Mtumba nje kidogo ya Jiji Dodoma.

 Mkurugenzi
wa Idara ya Watoto Mwajuma Magwiza wa Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii mara ya kuanza majukumu yake katika Ofisi Mpya
zilizoko Mtumba nje Kidogo ya Jiji la Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya
Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Leornard Mchau mara ya baada
kuanza majukumu yake katika Ofisi Mpya zilizoko Mtumba nje Kidogo ya
Jiji la Dodoma.

Share.

About Author

Leave A Reply