Friday, August 23

WAZIRI MKUU ASAINI MKATABA WA UWAZISHAJI WA SOKO LA PAMOJA KATIKA UMOJA WA AFRIKA

0


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepongeza makubaliano yaliyofikiwa na nchi za Afrika za kulifanya bara hilo kuwa eneo huru kibiashara.


Majaliwa aliyasema baada ya kumaliza kusaini mkataba wa nchi za Afrika kuhusu mkataba huo akimwakilisha Rais John Magufuli Jijini Kigali ambapo alisema Tanzania imeajiandaa vya kutosha kutekeleza mkataba huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali , Waziri Mkuu alisema Tanzania itahakikisha mkataba huo unatelekezwa bila kuathiri huduma zinazozalishwa ndani.

Alisema Tanzania itahakikisha mikataba mitatu ambayo imesainiwa inatekelezwa bila kuathiri uzalishaji na sera za ndani.

Mikataba iliyosainiwa na mataifa hayo 50 ya Bara la Afrika ni pamoja na mkataba wa kulifanya bara la Afrika kuwa eneo huru la biashara, Itifaki ya kisheria ya utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwamo uhuru wa makazi, haki ya kuishi na kufanyakazi popote bila vikwazo wala vizuizi vyoyote.

Azimio la tatu ni Azimio la Kigali ambalo limejumuisha mawazo ya uanzishwaji wa mchakato huo.

“Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Paul Kagame kwa kutilia maanani suala hili hadi kufikia hatua hii ya kusaini mkataba.

“Tanzania kama wadau wakuu wa mkataba huu tunakwenda kujipanga kuhakikisha mkataba huu unatekelezwa bila kusababisha vikwazo vyovyote.

“Hata hivyo tunakwenda kupeleka baadhi ya masuala haya katika vikao vya Baraza la mawaziri ili kuangalia sheria zetu zisije kuwa kikwazo katika utekelezaji wa mkataba huu.

“Kwa mfano Tanzania tunayo sera ya viwanda, lazima tuangalie ili tusije kuruhusu bidhaa kuingia nchini mwetu na kuathiri biashara na bidhaa zetu za ndani.

Vile vile katika uhuru wa biashara ya anga ambapo Tanzania bado tuna ndege chache ili tusije kuruhusu kiholela, l;azima tuwe waangalifu katika hilo.

“Aidha Tanzania tumeruhusu maeneo ya kuzalisha bidhaa, kwa hiyo lazima tuwe makini ili tusije kuruhusu na kuharibu mwenendo wa kiuchumi.

Awali akihutubia katika ufunguzi wa sherehe hizo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame aliyataja maeneo makuu ambayo mkataba huo umeangazia kuwa ni pamoja na eneo huru la biashara ya anga, miundombinu ya reli na barabara ambayo itaziunganisha nchi za Afrika kuwasiliana kwa urahisi.

Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), alisema mkataba huo unatoa nafasi maalum ya Ukanda wa Afrika kujali utu, kumnufaisha mkulima, mfanyabiashara na wabia wengine wa maendeleo kuja kutafuta fursa Afrika.

“Azimio hili linatoa nafasi kununu na kuuza bidhaa sambamba na kupata wabia duniani kote, biashara huru itatuweka pamoja na muafaka wa Afrika tutakayo” alisema Rais Kagame.

Mkataba huo ulisainiwa jana baada ya vikao vya maadalizi vilivyohusisha timu za wataalam na mawaziri wa biashara na mambo ya nje ya nchi zinazounda Umoja huo.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 50 wanachama wa AU ambao walisaini mkataba huo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.