Monday, August 19

WANAWAKE WA ARUSHA WAPEWA MKOPO WA MILIONI 120

0


Na Alice Mapunda, Arusha.
Wanawake wa Arusha watakiwa kutumia vizuri mikopo yao kwa kuwekeza kwenye shughuli  mbalimbali za maendeleo na zitakazo zalisha kwa wingi na kuwaletea mapato yakutosha katika familia zao.
Ameyasema hayo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Jenista Muhagama alipokuwa akikabizi hundi ya milioni 120 ya mkopo wa akinamama wajasiliamali, Jiji la Arusha.

Amewataka wanawake waonyeshe kuwa wanaweza kuinuka kiuchumi na kuacha utegemezi huku wakitekeleza majukumu yao katika ngazi za familia na jamii kwa ujumla.

“Mikopo hiyo mnayoenda kupewa ichukulieni kama mmepata tunda la embe katika mti wa miba,yani haitakaa itokee tena mkapatiwa mikopo hiyo kwa mara nyingine”.alisema

Aidha,amewahasa wakatumie vizuri  mikopo hiyo na waache kwenda kununua vitu ambavyo havitawasaidia katika kujiletea maendelea yao na familia zao.

Serikali ya awamu ya tano imelenga katika kuhakikisha matunda ya nchi yanaliwa na kila mtanzania,hivyo fursa hiyo ya wanawake kupatiwa mitaji kwa mikopo isiyo na riba nimkakati mzuri wakutelekeza ilani ya chama cha mapinduzi.

Amesema wizara yake ipo tayari kuwasaidia wakimama wote watakao fanikiwa kumaliza marejesho yao na atawasaidia kupata mikopo mingine ya riba nafuu huku wakiwa katika vikundi.

Pamoja na akimama kipatiwa hiyo mikopo wanaweza pia kutafuta fursa kubwa zaidi katika miradi mikubwa inayofanywa na serikali,ili na wao waweze kukua katika biashara zao.

Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa juhudi alizozifanya za kusaida makundi maalumu ya vijana,wanawake na wenye ulemevu katika kuwatengenezea ajira zaidi ya 200.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema akinamama ni kundi kubwa sana linalotegemewa kwa asilimia kubwa katika ngazi za familia na jamii kwa ujumla,hivyo aliona hana budi kutafuta namna yakuwawezesha ili waweze kujikwamua katika maisha yao.

Amewataka wenye mapenzi mema waendelee kusaidia akinamama katika Nyanja ya kujikwamua kiuchumi ile pale wanapokosa usaidizi basi waweze kusimama wao kama wao na kuendesha maisha yao na wategemezi wao.

Akisisitiza zaidi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,amesema mwanamke nisawa na hewa ya oxjeni pale inapokosekana inaleta maafa makubwa na pengine kupoteza kabisa uhai wa binadamu.

Akitoa salamu za pongezi  Mwenyekiti wa Tanzania Tour Operators (TATO) bwana Wilbad Chambulo kama mmoja wa wadau amesema alichofanya Gambo ni jambo la kuigwa na watu wengine na yeye atachangia kiasi cha milioni 20 ili wakimama wengine 100 waweze kukopeshwa.

Mikopo isiyokuwa na riba ya kuwezesha makundi mbalimbali katika Mkoa wa Arusha ilianza kwa vijana 200 kukopeshwa pikipiki na baada ya kufanya marejesho yao kiasi cha milioni 120 kimetolewa kuwakopesha akinamama 600 kama mtaji wakufanya  biashara mbalimbali.

 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Muhagama , Antony Mavunde na Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakikabidhi mfano wa Hundi ya Milioni 120 kwa akinamama 600, Jijini Arusha.
Baadhi ya Wadau na akinamama walioudhuria sherehe za kuwakabidhi mikopo akinamama 600 wa Jiji la Arusha.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.