Thursday, August 22

WANAWAKE WA ARUSHA WAPEWA MKOPO WA MILIONI 120

0


Na Alice Mapunda, Arusha.
Wanawake wa Arusha watakiwa kutumia vizuri mikopo yao kwa kuwekeza kwenye shughuli  mbalimbali za maendeleo na zitakazo zalisha kwa wingi na kuwaletea mapato yakutosha katika familia zao.
Ameyasema hayo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Jenista Muhagama alipokuwa akikabizi hundi ya milioni 120 ya mkopo wa akinamama wajasiliamali, Jiji la Arusha.

Amewataka wanawake waonyeshe kuwa wanaweza kuinuka kiuchumi na kuacha utegemezi huku wakitekeleza majukumu yao katika ngazi za familia na jamii kwa ujumla.

“Mikopo hiyo mnayoenda kupewa ichukulieni kama mmepata tunda la embe katika mti wa miba,yani haitakaa itokee tena mkapatiwa mikopo hiyo kwa mara nyingine”.alisema

Aidha,amewahasa wakatumie vizuri  mikopo hiyo na waache kwenda kununua vitu ambavyo havitawasaidia katika kujiletea maendelea yao na familia zao.

Serikali ya awamu ya tano imelenga katika kuhakikisha matunda ya nchi yanaliwa na kila mtanzania,hivyo fursa hiyo ya wanawake kupatiwa mitaji kwa mikopo isiyo na riba nimkakati mzuri wakutelekeza ilani ya chama cha mapinduzi.

Amesema wizara yake ipo tayari kuwasaidia wakimama wote watakao fanikiwa kumaliza marejesho yao na atawasaidia kupata mikopo mingine ya riba nafuu huku wakiwa katika vikundi.

 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Muhagama , Antony Mavunde na Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakikabidhi mfano wa Hundi ya Milioni 120 kwa akinamama 600,Jijini Arusha.
Baadhi ya Wadau na akinamama walioudhuria sherehe za kuwakabidhi mikopo akinamama 600 wa Jiji la Arusha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPARead More

Share.

About Author

Comments are closed.