Sunday, August 25

WALIOTUMIA JINA LA MAMA JANETH MAGUFULI KUTAPELI WAPANDISHWA KIZIMBANI

0


Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

WATU saba wakazi wa jijjini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu wanne tofauti wakikabiliwa na mashtaka mbali mbali likiwemo la kuchapisha taariza za uongo katika mtandao wa kijamii wa face book kwa kutumia jina la Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania, John Pombe Magifuli, mama Janeth Magufuli.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, Wanjah Hamza, Augustine Rwizile na Janet Mtega.

Akisomahati ya mashtaka wakili wa serikali Batlida Mushi amewataja washtakiwa hao kuwa ni,  Saada Uledi, Maftaha Shaban, Heshima Ally, Shamba Baila,Fadhili Mahenge, Obadia Kwitega na Stella Ommary.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde imedaiwa kuwa, Kati ya January 2017 na Machi 2019 jijini Dar es Salaam na maeneo mengine ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania washtakiwa  Saada, Shaban, Ally na Baila walikula njama ya kuchapisha maneno au taarifa za uongo kupitia ukurasa wao wa Facebook.

Katika shtaka la pili imedaiwa washtakiwa hao walichapisha machapisho katika ukurasa wao wa Facebook kuwa, Janet Magufuli ambaye ni mke wa Rais Magufuli ameunda Taasisi inayofanya kazi ya kukopesha  na kutoa mkopo kwa watu ikiwa na masharti yanayowataka watu hao kuweka fedha kama dhamana ya kupata mkopo huo.

Katika shtaka la tatu imedaiwa, kati ya Machi 2 na machine 8, 2019 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wakiwa kama waendeshaji wa ukurasa wa Facebook iliyosajiliwa kwa jina la Janeth Magufuli, kwa nia ya kudanganya na kupotosha na kwa kutumia mahamisho ya fedha kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine walijipatia  sh. Milioni 4,487,000/- kutoka kwa Simon Kunambi kama ulinzi/ dhamana ya mkopo ambao angepatiwa kutoka kwenye hiyo Taasisi ya Janeth Magufuli, huku wakijua kuwa siyo kweli.

Share.

About Author

Leave A Reply