Wednesday, August 21

TAMASHA LA WALI NAZI KUFANYIKA RAMADA RESORT HOTEL JIJINI DAR ES SALAAM

0 Mwazilishi wa Wali Nazi Food Festival, Helena Kapongo akizungumza na waandishiwa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha Tamasha la Wali nazi Food Festival litakalofanyika katika Hoteli ya Ramada Resort-Mbezi Beach jijini Dar es Salaam Aprili 2 mwaka huu.Mkurugenzi Mshirika wa Taasisi hiyo,  Salum Kihemba.
Afisa masoko Mwandamizi wa Ramada Hotel Resort Dar es Salaam- Mbezi Beach, Amina Kapya akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mshirika wa Taasisi hiyo,  Salum Kihemba. 
Mkurugenzi Mshirika wa Taasisi hiyo,  Salum Kihemba akizungumza na waandishi wa habar jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Wali nazi Food Festival litakalofanyika Aprili 2 mwaka huu katika hoteli ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam. Vyakula Vitakavyokuwepo ni Pamoja na Tamasha hili ni kwaajili ya Mabalozi pamoja na Wafanyabiashara mbalimbali hapa nchini. Kushoto ni Mwazilishi wa Wali nazi Food Festival, Helen Kapongo.
Afisa masoko Mwandamizi wa Ramada Hotel Resort Dar es Salaam- Mbezi Beach, Amina Kapya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la  Wali nazi Food Festival. Kushoto ni Mwazilishi wa Wali Nazi Food Festival, Helena Kapongo.

TAASISI ya Wali Nazi Food Festival  kwa kushirikiana na Ramada Resort Hotel  ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam imeandaa tamasha la chakula aina ya Wali Nazi na vyakula mbalimbali vya kiafrika litakalofanyika Aprili 2 katika hoteli  hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mshirika wa Taasisi hiyo,  Salum Kihemba amesema tamasha hilo ni la aina yake na kuwataka wananchi washiriki tamasha  hilo kwa chakula cha asili cha wali Nazi.

Amesema kuwa uzinduzi wa chakula hicho ni mdogo kwa kwani uzinduzi mkubwa utafanyika katika kipindi cha sikukuu ya Iddi na baada ya hapo watakwenda katika majiji matatu kwa ajili kuonyesha chakula bora cha wali nazi.

Kiingilio katika tamasha hilo ni sh.200,000 kwa mtu mzima na watoto chini ya 14 sh.100,000 ambapo  kwa watoto wa chini ya miaka sita watapata huduma mbalimbi bure kabisa. Kwa pamoja watapata burudani ya mziki  na chakula.

Kihemba amesema kuwa katika uzinduzi huo amealika mabalozi mbalimbali 30 pamoja na wafanyabishara 150 ikiwa ni kuweza kutangaza utamaduni wa nchi yetu.

Amesema baada ya kufanyika matamasha hayo watakwenda kutangaza katika mataifa mbalimbali chakula bora cha Wali Nazi.
Mwasisi wa Taasisi hiyo Hellena Kapongo amesema wamejipanga katika katika kutangaza utamaduni wa wa mtanzania katika chakula cha Wali Nazi.

Meneja wa Masoko Mwandamizi wa Ramada Resort Hotel, Amina Kapya amesema wanawakaribisha watu kushiriki tamasha hilo kutokana na walivyojipanga katika kutangaza chakula cha Kiafrika.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.