Wednesday, August 21

SHULE ZA AL MUNTAZIR, KSIJ KUTOA ELIMU K WA WATOTO WENYE UMRI WA ZAIDI YA MWAKA MMOJA HADI 18

0


SHULE za Al Muntazir zinaendeshwa chini ya mwamvuli wa KSIJ- Central Board of Education na hutoa  Elimu kwa watoto wenye umri kati ya mwaka mmoja na nusu hadi wenye umri wa miaka 18. 

Mifumo mbali mbali ya Elimu ya shule za Al Muntazir inaanzia wale wachanga tunawaita toodlers kuendelea Shule ya awali, msingi, sekondari na mwisho ngazi ya juu ya sekondari yaani A- levels.

 Shule za Al Muntazir zinasikia fahari kwani  hadi sasa zinatoa elimu kwa wanafunzi zaidi ya 4500 na kutengeneza ajira zaidi ya 400 za walimu na wasio walimu. Shule za Al Muntazir zinajulikana kwa kupenda kwao mafanikio na kupigania UBORA.

Moja kati ya miradi ambayo KSIJ- Central Board of Education imeanzisha kwenye hii miaka ya karibuni ni uendeshaji wa  shule ya wanafunzi  wenye mahitaji maalumu ya Al Muntazir kwa kifupi tunaiita (AMSEN) ambayo ilianza rasmi mwaka 2013, na kwa miaka 5 tu imefanikiwa kuelimisha wanafunzi zaidi ya  75.

AMSEN inatoa huduma hii ya Elimu  katika mazingira yenye madarasa na vifaaa vya kutosha na kukidhi mahitaji, chumba chenye nafasi na vifaa vya kutosha kwaajili ya (OT) Ocupational Therapy, speech na lugha, aqual therapy pool na uwanja wa michezo wa kutosha.

Shule hii ya watoto wenye mahitaji maalum AMSEN Wanatoa mafunzo na Elimu kwa watoto wenye ugumu katika kujifunza, usonji, dyslexia, Down Syndrome, Cerebral Palsy na nyinginezo za aina hizo.

Inahudumia watoto wenye umri kuanzia make 3 hadi 22.  Shule hii inatoa huduma ili kukidhi matarajio ya watoto hawa wenye mahitaji maalumu ili wajitahidi kufikia malengo yao katika harakati za kujipatia ajira kila mmoja kwa jinsi ya upekee wake alivyo umbwa na Mwenyezi Mungu.

Shule ya AMSEN iliyopo chini ya mwamvuli wa KSIJ- Central Board of Education imekua ikiandaa matembezi ya hiari  kwa muda wa miaka 4 mfulurizo ili kuweka alama ya siku ya usonji Duniani.Matembezi haya ni ishara ya juhudi katika kueneza ujumbe wa kuwafanya watu wote watambue na kuelewa kuhusu watoto wenye mahitaji maalumu.

Mwaka huu tena tumeandaa matembezi kwa mara ya 5  kwa kauli mbiu isemayo “TUWAPENDE NA TUWALINDE”

Kuwapenda na kuwalinda siyo tu kwa kuwaweka ndani na  kuwapa mahitaji mbali mbali wanayo hitaji, bali ni kwa kwa kuwapatia elimu na mafunzo ili waweze kujitegemea na kuonyesha ulimwengu kwamba wanaweza kufanya yote ambayo watoto wengine wa kawaida wanafanya napengine zaidi yao.

Na hiki ndicho ambacho haswa KSIJ Central Board of Eduacation ,kupitia shule ya watoto wenye mahitaji maalumu ya Al Muntazir imekua ikifanya na inataka watoto hawa wapate maisha yenye heshima na yaliyotulia.

Kwa mantiki hiyo basi napenda  kuwaalika   wazazi wakiambatana na watoto wao pamoja na umma yote ya watanzania popote walipo waungane nasi siku ya tarehe 25 Machi 2018 ili kutuunga mkono katika matembezi haya yatakayoanzia kwenye viwanja vya shue ya Msingi ya Al Muntazir Wavulana  iliyopo Barabara ya Barak Obama na kumalizikia kwenye viwanja vya shule ya msingi ya  Al Muntazir Wasichana iliyopo Barabara ya Umnoja  wa mataifa.

Naomba mtambue kuwa  peke yetu hatuwezi kufikia malengo BALI kwa  pamoja tutaweza.
NITATEMBEA KWAAJILI YA WATU WENYE USONJI WEWE JEeee?Read More

Share.

About Author

Comments are closed.