Monday, August 19

RC TABORA: WAKANDARASI WA KITANZANIA HAKIKISHENI MIRADI YENU INAKUWA YA KIWANGO CHA JUU

0


Na Tiganya Vincent
WAKANDARASI Kitanzania wametakiwa kuzingatia ubora, viwango  vya kazi zao ili waweze kuaminika kwa Serikali na hivyo kupata fursa kubwa ya kupewa miradi mipya inayotarajiwa kujengwa hapa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati alipokutana na ujumbe wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi(CRB)

Alisema ujenzi wa miradi chini ya kiwango na ambayo haidumu kwa muda mrefu kutawasababisha kutopewa kipaumbele pindi miradi inapokuwa ikitangazwa na badala yake miradi hiyo kutekelezw na wakandarasi wa kigeni.

Mwanri alisema ni vema wajenga tabia ya kushirikiana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ili waweze kuwa na nguvu kubwa na vifaa vingi ambavyo ndivyo vitawasaidia kuikamisha kwa wakati na kwa kiwango bora kinachotakiwa.

Alisema matokeo mazuri ya utekelezaji wa miradi yataifanya Serikali kutoa kipaumbele kwa Kampuni za Watanzania katika miradi ya ujenzi , jambo ambalo litawasaidia kujiimarisha zaidi.

Aidha Mkuu wa Mkoa aliwataka Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi aina mbalimbali kuzingatia suala la mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti kando kando ya miradi kama vile barabara , majengo pindi wanapokuwa wamekamilisha ujenzi wake.

Aliongeza kuwa katika maeneo yao ni vema wakawa na walau vitalu vya miche ya miti ili kuunga mkono juhudi za Serikali za utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa mistu
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri(kulia) akiagana jana na Meneja wa Wakala wa Barabarani Tanzania(TANROADS) Mkoani humo, Damian Ndabalinze (kushoto) mara baada ya mazungumzo yaliyolenga kujua hali ya ukarabati wa barabara zilizoharibiwa na mvua iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha kukatika kwa mawasilano katika njia mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri(kulia) akitoa maagizo jana kwa Mfanyakazi katika Kitalu cha Miche ya Miti mbalimbali cha Manispaa ya Tabora, Mariam Christopher(kushoto) na Meneja wa Wakala wa Mistu Tanzania (TFS) Manispaa ya Tabora Bakilana Mashauri (katikati) kuhusu kuotesha miti maji mingi kwa ajili ya kupanda katika maeneo mbalimbali katika Manispaa hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri(kulia) akitoa maagizo jana kwa Meneja wa Wakala wa Mistu Tanzania (TFS) Manispaa ya Tabora, Bakilana Mashauri (kulia) kuhusu kuotesha miti maji mingi kwa ajili ya kupanda katika maeneo mbalimbali katika Manispaa hiyo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.