Sunday, August 18

POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI

0


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi nchini limesema hali ya usalama nchini ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua kwa kiasia kikubwa huku likieleza kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu

Taarifa iliyotolewa leo jijii Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ,IGP Simon Sirro ameshukuru ushirikiano ambao wananchi wanautoa kwa jeshi hilo ambao umesaidia kupunguza matukio ya uhalifu na nchi kiusalama iko shwari.

“Kiujumla hali ya usalama hapa nchini ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa na jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili  kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia,”amesema.

Kuhusu maandalizi ya jeshi hilo kuelekea Pasaka,Sirro amesea wamejipanga katika mikoa yote na kuwahakikishia wananchi kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha Sikukuu hiyo inasherekewa kwa amani na utulivu.

“Na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo katika hali ya  utulivu,”amesema.

Amewaomba wazazi na walezi kuwa waangalifu kwa watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu.”Kwa wanaomilii kumbi za starehe wanatakiwa  kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi”.

Wakati huohuo Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.