Saturday, August 24

Polisi Ubungo waendesha mafunzo kwa madereva

0


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Mkuu wa kituo cha ukaguzi wa Magari katika kituo cha Mabasi Ubungo Terminal Ibrahim Samwix ameendesha mafunzo kwa madereva wa Magari makubwa kwa lengo la kufanya utambuzi wa gari n breki.

Akizungumza na Madareva hao jana jijini Dar Es Salaam.katika.kituo hicho cha Ubungo Terminal alisema mafunzo hayo ni endelevu kwa madereva ili kuwajengea uwezo wa kutambua mifumo ya gari jinsi linavyojiendesha.

 Alisema mafunzo hayo ni bure na wataendelea kuyatoa Mara kwa Mara kwa madereva wa mikoani  na nje ya nchi kwa lengo kupumbunguza au kuondoa ajari za barabarani.

Ibrahim alisema madereva watapewa vyeti baada ya kufanya mafunzo hayo Mara kwa Mara na yeye kama mkufunzi amefanya kazi hiyo kwa kujitoa zaidi.

“Nafanya kazi hii kwa kujitolea ili kuhakikisha madereva wanapata uelewa na kuepuka kugombana na askari wa barabarani Mara kwa Mara.” Alisema Ibrahim.

Pia alitoa rai kwa madereva kuepuka kufanya mashindano barabarani kwani kufanya hivyo nimuhatarisha usalama wao na usalama wa abiria waliowabeba.

 Ibrahimu alisisitiza kwa kuwataka maderava kuhakikisha wanashiriki kikamilifu mafunzo hayo ili waweze kupata uelewa zaidi na kufanya kazi yao kwa kujiamini zaidi.

 Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi cha Mabasi Ubungo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akiendesha mafunzo kwa madereva ikiwa ni hatua ya kupunguza ajali za Barabarani zitokanazo na makosa ya kibinadamu.

 Madereva wakipata elimu kabla ya kuanza safari

Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akionesha madereva namna ya matumizi ya Blake katika mafunzo hayo yaliyofanyika ofisini saa 10 alfajiri.

Share.

About Author

Leave A Reply