Sunday, August 18

POLISI KANDA MAALUM DAR YAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA

0


*Kamanda Mambosasa agusia upelelezi kifo cha Akwilina 

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

KAMANDA wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema  hali ya usalama wa Jiji kuelekea Sikukuu ya Pasaka na wamejiimarisha kulinda usalama wa raia na Mali zao.

Mambosasa ameeleza kuwa Jeshi limejipanga kwa kuimarisha ulinzi na kuhakikisha wakazi wa jiji la Dar es salaam wanasherekea vizuri sikukuu hii.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Mambosasa ameeleza hakuna mtu yeyote atakayepata fursa ya kufanya tukio lolote la kiharifu kwani jeshi limejipanga kwa doria ya miguu, mbwa, pikipiki, farasi na magari yote yaliyopo katika kuhakikisha usalama wa raia wote na pia wameongeza nguvu ya ulinzi katika fukwe zote.

Kuhusu disko toto Mambosasa amesema kuwa hakuna kibali kilichoombwa hivyo hategemei kuona kumbi yoyote itakayokusanya watoto.

Kuhusu mauaji ya Akwilina Akwilini kamanda Mambosasa ameeleza upelelezi bado unaendelea na maelezo waliyoyapata bado wanayafanyia kazi uchunguzi ukikamilika watatoa maelezo.

Ametoa rai kwa waendesha vyombo vya moto kuwa makini na kuepukana na ulevi ili kulinda usalama wao na wananchi kwa ujumla.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.