Monday, August 19

Mwenyekiti wa Chadema na viongozi wengine wa chama hicho wapelekwa mahabusu kwa kukosa Dhamana, Hatma yao kujulikana Ijumaa machi 29

0


 Mwenyiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa katika gari ya Polisi tayari kwa kupelekwa Segerea baada ya kukosa Dhamana katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kutokana na Mashtaka yanayo wakabili.
  Mwenyiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho (Zanzibar) Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Bara) na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini , Ester Matiku wakiwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu mkazi kisutu baada ya kesi yao kuarishwa na kuamuriwa kurudi rumande bila dhamana.

*Mahakama yaamua kuwanyima dhamana kwa usalama wao
*Hatma yao kujulikana Ijumaa iwapo watatoka mahabusu au la

Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho ambao wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wamepelekwa mahabusu baada ya upande wa Jamhuri kuwasilishwa maombi ya kuwanyima dhamana.

Mbali ya Mbowe wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Bara Salum Salum, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent Mashinji.
Hivyo ni baada ya kusikilizwa mabishano marefu ya upande wa Jamhuri na ule wa utetezi juu ya dhamana ya washtakiwa kama wapate au la, mahakama imesema itatoa uamuzi Machi 29 mwak huu, mshtakiwa Mbowe na wenzake wamepelekwa rumande.

Mapema upande wa Jamhuri uliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kunyimwa dhamana kwa washtakiwa kwa njia ya mdomo.
Akiwasilisha sababu za kupinga dhamana mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Mkuu Dk. Zainabu Mango amedai  ni kwa sababu za usalama wa jamii na nchi kiujumla kama ilivyoelezwa kwenye hati ya mashtaka.

Amedai wanatambua dhamana ni haki ya mshtakiwa lakini hakuna haki isiyokuwa na wajibu kwa mujibu wa katiba ya nchi. Kwani Mashtaka yao wanaashiria kutokutii amri yao kikatiba, utekelezaji wa haki binafsi unapaswa kuzingatia haki za watu wengine.

Alidai alidai kwamba makosa yanayowakabili yanahatarisha usalama nchi na kuwapa dhamana ni kuendelea kuwapa nafasi ya kuendelea kufanya makosa hayo.

“Jukumu la dhamana liko chini ya mahakama hii. Hata  hivyo kabla ya mahakama kutumia mamlaka yake kutoa ama kuzuia dhamana inapaswa kuangalia mazingira ya kosa husika”, amedai Dk.mango. Ameiomba Mahakama kuzingatia maslahi ya umma kwa ujumla wake kwa hatari ya makosa wanayoshtakiwa nayo na usalama wa taifa.

Wakili Faraja alidai kuwa kama washtakiwa wataruhusiwa kurudi uraiani baada ya matamko hayo ni wazi kwamba haki ya upande wa pili itapotea, matamshi yaliyotolewa na washtakiwa yana madhara endelevu kwa watanzania kwani tuna taarifa za upelelezi kwamba baadhi ya mambo yaliyoongelewa, ushawishi uliotolewa unaonekana kuna utekelezaji wa kihalifu.
Akijibu hoja hizo Wakili wa utetezi Peter Kibatala amedai hakuna chochote cha kisheria kilichozungumzwa kutoka kwenye dawati, kilichoko mbele ya mahakama sio maombi ni pingamizi la dhamana na hakuna ushahidi wowote kwa yaliyosemwa.
Pia Kibatala amedai Wakili anashindwa kutofautisha askari mpelelezi na mawakili wasomi na Mahakama haiwezi kumnyima mtu dhamana kwa taarifa ambazo haziko mahakamani. Aliendelea kudai  hati ya mashtaka haina jina wala sahihi ya aliyeandaa jambo ambalo limekatazwa na Mahakama Kuu.

 Mwenyiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji, Peter Msigwa, Kaimu katibu Mkuu wa Chama hicho Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba , John Mnyika , Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini , Ester Matiku wakiwa wamekaa katika benchi la mahakama ya hakimu mkazi kisutu kusubiri kusomewa mashtaka yao
 Mwenyiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji, Peter Msigwa, Kaimu katibu Mkuu wa Chama hicho Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba , John Mnyika , Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini , Ester Matiku wakipandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.

Baadhi ya viongozi wa Vyma vya Siasa na wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya mahakama kusuburi kushuhudia msafara wa viongozi wakuu wa Chadema wakipelekwa Rumande


Kusoma zaidi BOFYA HAPARead More

Share.

About Author

Comments are closed.