Tuesday, August 20

MJASIRIAMALI ATUSUA MAMILIONI YA SHINDA NA UMOJA SWITCH.

0


Afisa Masoko wa Umoja Swich,(Beatrice Emmanuel) akimkabidhi Nd, Muhunzi Kisome,(Kushoto) zawadi ya fedha taslim shil.Mil. 1 alizoshinda katika droo ya pili ya shinda na Umoja Swich

Kapuni ya Umoja switch imewazawadia washindi wake zawadi walizoshinda kwenye droo ya pili ya Shinda na Umoja Switch iliyochezeshwa February 2 mwaka huuKatika droo hiyo ya pili ilitoa washindi katika vipengele vinne ambavyo ni, washindi wawili wa fedha taslimu Milioni moja, mshindi wa fedha taslim mara mbili ya muamala aliyofanya kwenye ATMs za UmojaSwitch, washindi wanne wa Simu za mkononi (Smart phones) na washindi zaidi ya 20 wa T-shirt za UmojaSwitch
Akiwakabidhi zawadi hizo za afisa masoko wa Umoja Switch Umoja Beatrice Emmanuel amesema anawashukuru wateja wa Umoja Switch kwa kuendelea kutumia kadi za Umoja Switch na amewataka wale ambao hawajabadili kadi zao wafike kwenye Benki zao ili kubadilisha kadi zao na waingie kwenye droo ya Pili ya Promosheni hii ya Shinda na Umoja Switch
Felister Japhet, akipokea zawadi yake ya simu ya mkononi(smart phone) toka kwa Afisa masoko waUmoja Swich Beatrice Emmanuel , aliyoshinda katika droo ya pili ya shinda na umoja switch
Akizungumza na Fahari News kwa niaba ya washindi wenzake Bwana Muhunzi Kisome ambae ndio mshindi wa Milioni moja, mfanya biashara kutoka Chamanzi Jijini Dar es salaam amesema hakutegema kama angekuwa mshindi wa fedha hizo na wakati amepigiwa simu alipuuza mpaka alipoamua kujidhihirishia kwa kuangalia kama kweli kuna Droo ya Shinda na Umoja Switch inayochezeshwa kupitia Simu yake 
“kiukweli siku amini mara ya kwana mpaka nikaingia kwenye internet kuhakikisha, walivyonipigia simu mara ya pili ndo nikafika hapa na nimeamini baada ya kuona na waandishi wa habari wapo hapa, pesa yangu nitaifanyia kitu ambacho kitakua ni kukbukumbu na shukrani kwa kampuni ya UmojaSwitch” alisema Kisome
fisa Masoko wa Umoja Switch, Beatrice William akiwa pamoja na baadhi ya washind wa droo ya pili ya shinda na Umoja.
Kampuni ya umoja Switch imekua ikitoa huduma za kifedha kwa kushirikiana na mabemki zaidi ya 20 nchini kwa njia ya kielectronic ili kuwarahisihia wateja wa mabenki njia rahisi za kufanya miamala kwa kutumia ATMs za Umoja Switch zilizosammbaa Tanzania NzimaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.