Monday, August 19

MILIONI 400/= KUJENGA MAJENGO MANNE YA KISASA

0


Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imepokea fedha kutoka  Ofisi ya Raisi TAMISEMI kwa ajili ya kuongeza majengo katika kituo cha afya Namtumbo.
Ofisa Habari wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo, Yeremias Ngerangera alisema kuwa Halmashauri hiyo ilipokea fedha hizo mwezi Novemba mwaka 2017 na baada ya kupokelewa kwa fedha hizo  Halmashauri ilipitia miongozo ya matumizi ya fedha hizo ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa.
Aidha Ngerangera aliongeza kuwa baada ya kupitia miongozo ya matumizi ya fedha hizo Halmashauri imeanza ujenzi wa majengo hayo  manne katika kituo cha afya Namtumbo kilichopo katika kata ya Rwinga mjini Namtumbo.

Injinia wa majengo Katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo, Hasssani Kinonono aliyabainisha majengo yanayojengwa kuwa  ni pamoja na Jengo la upasuaji, Jengo la wodi ya akina mama wajawazito,Maabara na Nyumba ya waganga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Christopher Kilungu alidai kuwa kutakuwa na ukarabati wa jengo la kuhifadhia maiti  pamoja na kujenga kichomea taka kwa kutumia fedha zitakazo baki katika ujenzi wa majengo hayo manne.
Kilungu pamoja na mambo mengine alidai kuwepo na salio katika ujenzi huo wa majengo manne lililotokana na ujenzi huo kutumia  akaunti ya nguvu ya jamii( Force account) na kusaidia kupunguza matumizi makubwa ya fedha hizo na kuwa na salio linaloweza kufanya kazi ya kukarabati chumba cha maiti na kujenga kichomea taka katika kituo hicho.
Kituo cha afya Namtumbo kina wodi ya watoto,wodi ya wagonjwa ,jengo la upasuaji kwa akinamama wajawazito na jengo la kuhudumia wagonjwa wan je  ambapo kwa sasa ujenzi huo utasaidia kuboresha huduma za jamii katika kituo hicho cha Afya.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.