Sunday, August 25

Mchungaji kizimbani kwa kusafirisha dawa za kulevya

0


Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
 Mchungaji Henry Ogwany (44),  raia wa Nigeria na wenzake watatu,  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini zenye uzito wa zaidi ya kilogramu 19.

 Mchungaji Ogwanyi, amepandishwa kizimbani pamoja na mshitakiwa mwengine, Onyebuchi Ogbu (34), raia wa Nigeria anayeishi eneo la Msimbazi,  ambao kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi huku washitakiwa wengine aliopandishwa nao kizimbani mchungaji huyo ni raia wawili wa Lativia, Linda Mazure (21) ambaye ni mwanafunzi na Martins Plavins (20), mkandarasi na mkazi wa Lativian na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwizile.

Mbele ya Hakimu Rwizile, imedaiwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula akisaidiana na Batilda Mushi kuwa Aprili 17, 2019,  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) washitakiwa Mazure, Ogwanyi na Plavins walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilogram 4.87.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, washitakiwa hawakiruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka  ya kusikiliza kesi huyo hadi Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) atakapotoa kibali.

Kwa mujibu wa  upande wa mashitaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 7, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.

Mbele ya Hakimu mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Wakili wa Serikali Batilda Mushi amedai kuwa, Ogwany na Ogbu wote ni wafanyabiashara na wakazi wa Nigeria na Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Amedai, Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Msimbazi wilayani Ilala jijini humo washtakiwa hao walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroini zenye kilogramu 15.8.

Hakimu Shaidi amesema washitakiwa hawaruhusiwi kujibu chochote kwa saba mahakama hiyo haina mamlaka na kwamba mashitaka wanayoshitakiwa nayo hayana dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 7, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Share.

About Author

Leave A Reply