Friday, August 23

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UJENZI WA SEKONDARI MICHEWENI

0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Kaskazini Pemba kushirikiana katika shughuli za maendeleo. 

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha Afya cha Huduma ya Mama na Mtoto Shumba Vyamboni wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. 

Kituo hicho cha Mama na Mtoto cha Shumba Vyamboni kitatoa huduma za Mama na Mtoto ambapo jumla ya Wananchi 5,593 wakiwemo wanawake wenye uwezo wa kuzaa 1543 na watoto chini ya umri wa miaka mitano 984 watapata huduma bora ya uzazi, lishe na ustawi wa mama na mtoto. 

Vijiji vitakavyofaidika na huduma ya kituo hicho ni pamoja na Kibubunzi, Kikunguni, Mihogoni, Nyuma ya Mti, Mgeninje, Utaani, Shumba vya Mboni, Uwondwe, Mamoja, Gombe, Uwaani na Bule. 

Katika ziara hiyo yenye lengo la kuhimiza shughuli za maendeleo Makamu wa Rais alikagua ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Micheweni pamoja na kumtembelea Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi Bi. Mrashi ambapo alimkabidhi mabati ya kuezekea nyumba yake inayojengwa na wanachama wa chama cha Mapinduzi katika eneo la Sizini. 

Mwisho Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM la Ukunjwi ambapo aliwaambia wakina Mama kuwa mstari wa mbele katika kuonesha njia ya kuwa kiongozi bora. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwonekano wa ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba
Read More

Share.

About Author

Comments are closed.