Sunday, August 25

MAHAKAMA YAAMURU MMILIKI IPTL AKATIBIWE HOSPITALI YA MUHIMBILI

0


Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Sethi, kupelekwa  kutibiwa  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).

Uamuzi huo umetolewa  Hakimu Mkazi Mkuu wa,  Huruma Shaidi, baada ya mshtakiwa kudai kuwa anaumwa na anatakiwa kwenda kutibiwa ili aweze kuendelea na kesi.

Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi ameyasema hayo leo Machi  29/2018 baada ya mshtakiwa kudai kuwa anaumwa sana.
“Mheshimiwa hali yangu imaribika sana naitaji kupatiwa matibabu”, amedai Sethi.

Hata hivyo, baada ya Seth kutoa ombi hilo la matibabu, Wakili wa Serikali, Leornad Swai alidai ni kweli mshtakiwa huyo anaonekana ni dhaifu lakini aliiomba mahakama taratibu za Magereza zifuatwe. 

” Tutawasiliana na magereza waweze kumtibu kwa utaratibu wa serikali”, amedai Swai.

Baada ya kudai hayo Hakimu Shaidi amesema, 

“Mshtakiwa ni kweli anaunwa, huhitaji kuwa na daktari kujua mtu anaumwa kwa kumuangalia tu anaonekana, hatuwezi kutenda haki kama mtu ni mgongwa, naamuru apelekewe Muhimbili akatibiwe aweze kuendelea na kesi”, amesema Shaidi.

Mapema Wakili wa Takukuru,  Pendo Temu akisaidiana na Swai,  alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri bado haujakamilika.

Alidai, wanafanya mawasiliano na nje ya nchi kupata nyaraka muhimu katika kikamilisha upelelezi. 

Pia ameomba kwenda kuchukua maelezo ya mshtakiwa namba mbili, Seth, afya yake itakapoimarika.

kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 11, mwaka huu itakapotajwa.

Seth na James Rugemarila wanakabiliwa  wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.bilioni 309.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.