Wednesday, August 21

MADIWANI MANYARA WALALAMIKIA KUKATWA POSHO ZAO

0


MADIWANI wa Mkoa wa Manyara, wamesikitishwa na kitendo cha Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwahoji kila mara na kuagiza
warudishe posho walizochukua jambo linalosababisha wavunjike moyo wa
kufanya kazi zao.

Wakizungumza mjini Babati kwenye kikao cha jumuiya ya serikali za
mitaa (Alat) cha mkoa huo, madiwani hao wameazimia kuonana na mkuu wa
mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ili kuongelea jambo hilo.

Mwenyekiti wa Alat wa mkoa wa Manyara, George Bajuta alisema kitendo
cha Takukuru kuwahoji madiwani na kuagiza warudishe posho walizochukua
siyo sahihi kwani jambo hilo lingepaswa kuachwa.

Bajuta alisema kasoro zilizojitokeza kwenye baadhi ya halmashauri
zisitumike kuwaadhibu madiwani wengine ambao hawastahili kwani hata
posho zenyewe zinazotolewa kwao ni kidogo.

“Wabunge wanapatiwa mishahara mikubwa na posho nzuri sasa baadhi
walipendekeza kuwa madiwani wanafuja fedha hivyo kusababisha hali hii
ya udhalilishaji kujitoleza,” alisema.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Jackson Sipitieck
alisema kuna haja ya mkuu wa mkoa huo, katibu tawala wa mkoa, kamanda
wa Takukuru na mkuu wa usalama wa taifa wa mkoa, kukutana nao ili
kujadili tatizo hilo.

Mjum

be wa Alat wa mkoa huo, Daines Peter alisema maslahi na haki ya
madiwani ibaki palepale kwani wana majukumu mengi kwa ajili ya
kutumikia wananchi.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel
alisema maslahi ya madiwani ni madogo lakini wanajitolea ila suala
hilo linawavunja moyo.

wenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Babati, Nicodemus Tarmo alisema
hata Rais John Magufuli aliwahi kusema kwenye kikao cha Alat Taifa
kuwa posho za vikao wanazopokea madiwani kupitia utaratibu uliowekwa
uachwe.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu vijijini, Joseph Mandoo
alisema vikao vya madiwani vya vyama na vya kumchagua Makamu
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya wanapaswa kulipwa kwani ni
maandalizi ya kikao cha baraza la madiwani.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mbulu, Gidishanga alisema wabunge
hawatetei tena maslahi ya madiwani ila mbunge wa jimbo la Chemba, Juma
Nkamia amekuwa akiwasemea madiwani bungeni.

Katibu tawala msaidizi wa mkoa huo (serikali za mitaa) Kenedy Kaganda
alisema kila diwani anapatiwa posho zake kulingana na stahili zake
ikiwemo fedha za kujikimu.

Hata hivyo, kaimu mkuu wa Takukuru mkoani Manyara, Isdory Kyando
alisema madiwani waliotakiwa kurudisha posho ni wale waliochukua miaka
iliyopita na sasa bila kustahili kuzichukua.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Leskar Sipitieck (katikati) akiandika yanayozungumzwa kwenye kikao cha Alat cha mkoa huo, kilichofanyika mjini Babati, kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Joseph Guulo Mandoo.

 Mwenyekiti wa Alat wa Mkoa wa Manyara, George Bajuta akizungumza wakati akifungua kikao cha Alat cha mkoa huo kilichofanyika mjini Babati.

Baadhi ya wajumbe wa Alat wa Mkoa wa Manyara, wakifuatilia kikao chao
kilichofanyika mjini Babati.

Share.

About Author

Leave A Reply