Tuesday, July 23

Mabinti watakiwa kutumia tehama kuondoa changamoto katika jamii

0


Na mwandishi wetu

KAIMU Balozi wa Marekani nchini Dk.  Inmi Patterson amewataka mabinti wa Tanzania kufikiria taifa lao na namna ambavyo wanaweza kusaidia kuondoa changamoto mbalimbali zinazokabili jamii yao.

Kauli hiyo ameitoa katika jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali lililoshirikisha mabinti wa sekondari wa mkoa wa Dar es salaam; pamoja na mambo mengine walishiriki katika shindano la ubunifu wa programu za kompyuta.

Jukwaa hilo linalojulikana kama Girls Entrepreneurship Summit (GES) 2018 linachagiza mabinti kutumia Tehama kutatua matatizo yaliyopo katika jamii.

Jukwaa hilo lililoandaliwa na ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini limelenga kusaidia mabinti kuchangia utatuzi wa matatizo kwa kuwa wabunifu katika ujasiriamali.

Kaimu Balozi huyo aliwataka mabinti hao kuwa na uvumilivu katika kukabiliana na changamoto zilizopo na kujenga mtandao ambao utawasaidia kuendelea mbele zaidi kiuchumi.

Alisema mtaji mkubwa wa wajasiriamali ni ubunifu na wazo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi bila kuogopa changamoto zilizopo.

 Mapema katika hotuba yake Mwanzilishi mwenza wa Apps &Girls, Carolyne Ekyarisiima alisema kwamba jukwaa hilo na mashindano hayo yamelenga kuhakikisha kwamba binti anawezeshwa katika ulimwengu wa kidijiti  kwa kumsogezea vishawishi mbalimbali vinavyompa motisha kuwa mbunifu kwa kutumia tehama.

Share.

About Author

Leave A Reply