Monday, August 19

KUWAFUNGIA NDANI WATOTO WENYE USONJI NI KUWANYIMA HAKI YA KUPATA ELIMU-DK TULIA ACKSON

0


 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Spika , Dk. Tulia Ackson amesema wazazi wasiwafungie watoto wao majumbani kutokana na maumbile yao kufanya hivyo ni kuwakosessha haki ya kupata elimu.

Dk. Tulia ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani yaliyofanyika katika shule ya Almuntazir  jijini Dar es Salaam, amesema kuwa watoto wenye mahitaji maalum wana uwezo mkubwa hivyo ni lazima wazazi wachukue jitihada za kuwapatia elimu.

Dk. Tulia amesema kuwa hakuna ubaguzi mbaya kama kuwabugua watu wenye mahitaji maalumu kwani kutokea kwao huko ni mipango ya Mungu  ambayo binadamu hawezi kuzuaia.

Amesema jitihada ya shule ya Almuntazir kusomesha watoto wanafunzi wenye mahitaji maalum ni jambo la msingi wanalolifanya ikiwemo kupunguza nusu ya asilimia ada katika shule hiyo kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Aidha aliitaka shule hiyo kuanzisha huduma ya mabweni ili kuwawezesha wanafunzi wenye uhitaji huo.  

Dk. Tulia amesema shule zingine ziige mfano wa Almuntazir katika kuwa mpango wa kutoa  elimu kwa wanafunzi wenye mahiataji maalum.

Nae Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema serikali inaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Almuntazir katika utoaji elimu katika kundi lenye mahitaji maalum.

Amesema kuwa watu wenye mahitaji maalum wana uwezo mkubwa ambapo wakipata elimu wana uwezo kushangaza dunia kutokana na ubunifu wao.

Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi ya Central of Education, Imtiaz Lalji amesema ameiomba serikali na sekta binafsi kutoa kipaumbele cha ajira kwa watu wenye sifa lakini ni watu wenye mahitaji maalum.

Amesema kufanya hivyo kutafanya wanafunzi wenye mahitaji kujituma kutokana na kuwa na uhakika wa jaira pindi wanapohitimu kozi mbalimbali katika vyuo vilivyopo nchini.

Amesema kwa mwaka mtoto mmoja mwenye usonji hutakiwa kulipa ada ya Milioni Sita na kuongeza kuwa hadi sasa wana wanafunzi 80.

“Kwa mwaka mtoto mmoja anatakiwa kulipa Milioni sita lakini sisi tumekuwa tukichangia Tatu na mzazi wake analipa inayobaki” alisema Ladak. 
 Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matembezi ya kilomita moja katika siku maadhimisho ya siku watu wenye mahitaji maalum Duniani yaliyoanzia katika Shule ya Msingi  Almuntazir mpaka Shule ya Sekondari  Almuntazir, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akiwa na watoto wenye mahitaji maalum katika matembezi ya maadhimisho ya siku watu wenye mahitaji maalum Duniani yaliyoanzia katika Shule ya Msingi  Almuntazir mpaka Shule ya Sekondari  Almuntazir ,jijini Dar es Salaam.
 Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akizungumza katika maadhimishio ya watu wenye mahitaji maalumu duniani yaliyofanyika katika shule ya Almuntazir ,jijin Dar es Salaam .
 Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile akizungumza hatua ya serikali katika kuunga mkono jitihada za wadau wanaojitolea kutoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Central of Education, Imtiaz Lalji akizungumza jinsi wanavyotoa elimu kwa wanafunzi wa wenye mahitaji maalum katika shule za Almuntazir jijini Da es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shule za Almuntazir, Mahmood Ladak akizungumza na waandishi habari elimu wanayotoa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum akiwa na wabunge ambao wameitikia wito katika kuhamasisha jamii kuhusiana na utoaji wa elimu kwa wanafunzi wenye mahaitaji maalum ,jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akikabidhiwa  zawadi na mjumbe wa bodi wa Khoja Jamaat, Azim Dewj katika maadhimisho ya siku watu wenye mahitaji maalumu leo jijini Dar es Salaam.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.