Thursday, August 22

KAMPUNI YAJITOSA KUSAKA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO

0


Na Said Mwishehe,  Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Carrer Times Ltd inayoshighulisha na teknolojia imeandaa Africa Technology Awards yenye lengo la kusaka na kuibua wabunifu katika mambo yanayohusu teknolojia na hasa ya habari na mawasiliano nchini.

Imesema kuna vijana wengi ambao wanao uwezo wa kubuni mambo yanayoweza kusaidia maendeleo ya nchi, hivyo wameamua kuchukua jukumu hilo kwa kutoa tuzo hiyo baada ya kushindanisha kazi za ubunifu ambazo washiriki watazionesha kwao.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Carrer Time Ltd Hawa Hongo amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa watatoa tuzo hiyo baada ya kupata washindi kwenye mambo ya ubunifu na kuanzia kesho wataanza kutoa fomu kwa wanaotaka kushiriki.

“Tunafahamu kuna vijana wengi ambao wapo mtaani na wanao uwezo mkubwa katika kubuni mambo yanayohusu teknolojia na hao ndio ambao tunawataka kuwaibua kwa maslahi ya nchi yetu.Tunaka vijana ambao wataoesha uwezo wao halisi katika mambo ya ubunifu,”amesema.

Amesema kumekuwepo na mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yakiibua vipaji lakini kwenye mambo ya ubunifu katika mambo yanayohusu teknolojia haifanyiki sana na hivyo wao kupitia kampuni yao wameamua kusaka vijapaji vilivyojificha mtaani.

Kuhusu taratibu za kupata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano hayo, amesema wataanza kutoa fumu ambazo zitakazokuwa zinatolewa kwenye ofisi zao zilizopo Mikocheni B mtaa wa Huruma jijini Dar es Salaam.

“Kwa walio Dar es Salaam fomu watakuja kuchukua ofisini kwetu na wale wa mikoani wanaotaka kushiriki  watachukua fomu kupitia barua pepe africantechweek@gmail.com.Muda wa kuchukua fomu utakuwa wa kuanzi kesho hadi mwezi wa nne na mwezi wa tano ndio shindano litafanyika na kuwapata watakaoshinda tuzo ambayo tutaitoa kwa ajili yao,”amesema Hongo.

Amesema wanaamini baada ya mashindano hayo kukabidhi tuzo kwa washindi katika ubunifu wa mambo ya teknolojia itatoa fursa kwa vijana hao kutambulika na kubwa zaidi kupata ajira kwa kampuni na taasisi mbalimbali ambazo zitafurahishwa na ubunifu utakaoonekana.

“Kampuni yetu inafahamu kuna vijana wengi ambao hawakubahatika kwenda shule au chuo lakini wana vipaji vya hali ya juu katika mambo ya ubunifu. Hivyo wakibainika itakuwa rahisi kuwawezesha kufanya kazi zao vizuri na sisi tutakuwa mabalozi wao katika kuelezea ubunifu wao,”amesema.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Carrier Time Ltd, Hawa Hongo akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari alipokuwa anazungumzia Africa Teknology Awards 2018 itakayotolewa na kampuni yao Mei mwaka huu kwa washindi wa shindano la ubunifu katika mambo ya teknolojiaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.