Sunday, August 25

KAMPUNI YA DATA VISION KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPELEKA NCHI KWENYE UCHUMI WA KATI

0


Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
KAMPUNI ya International Data Vision inayohusika na masuala ya Utafiti, imeahidi kushirikiana na Serikali ili kuifikisha nchi kwenye uchumi wa viwanda.

Ahadi hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Geofrey  Maclean wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Pia amesema licha ya kueleza mafanikio ya shirika hilo ameeleza mbinu mkakati za kiubunifu  za kutofanya biashara kimazoea na hiyo ni kwa kuhusisha matumizi ya teknolojia(ICT) na tafiti mbalimbali na kujua mahitaji ya soko la dunia.

Aidha ameomba ushirikiano wa wafanyakazi na watu wanaowafikia katika maeneo mbalimbali.

Kuhusu kushirikiana na Serikali katika kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati Mwaijonga ameeleza wanaunga mkono dhamira hiyo na wanashiriki kwa namna mbalimbali kama vile kulipa kodi stahiki kwa Serikali, kutengeneza ajira na kuleta ubunifu mpya katika biashara.

Pia Mwaijonga amesemaleza wana mpango mpya wa kusafirisha maarifa (skills)ili  zikatumike katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuiongezea nchi kipato kitakachosaidia kuifikisha kwenye uchumi wa kati.
 Mkurungenzi  Mtendaji wa Kampuni  ya Data Vision International, Geofrey  Maclean Mwaijonga aizungumza na wafanyaazi wa kampuni hoyo  katika maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
 Wafanyaazi wa kampuni  Data Vision International  wakimsikiliza Mkurungenzi  Mtendaji wa Kampuni hiyo, Geofrey  Maclean Mwaijonga wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo yaliyofanyika jijini Dar es SalaamRead More

Share.

About Author

Comments are closed.