Monday, August 19

JUMUIYA YA WAZAZI ILALA WAAMUA KUWA WALEZI SHULE YA MSINGI MCHIKICHINI

0


 JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imechukua jukumu la kuwa mlezi wa Shule ya Msingi Mchikichini ili kupunguza changamoto zinazoikabili shule hiyo.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam  na Katibu wa Elimu ,Malezi   na Mazingira (EMA)Wilson Tobola  wakati wa maadhimisho ya wiki ya Wazazi Ilala.

Tobola aliingia jukumu hilo la kuwa mlezi na kuahidi kumaliza changamoto za shule hiyo baada kuona ina  uhaba wa kadhaa vifaa vya Steshenali, na uzio wa shule.

 ” EMA leo tunadhimisha wiki ya wazazi kwa kugawa vifaa vya shule vya thamani ya Sh. 700,000  katika shule hii vilivyotolewa Azim Khan ambaye ni  Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa Dar es Salaam ili kusaidia wanafunzi wa Mchikichini” amesema Tobola .

Tobola pia ambaye ni mlezi wa shule hiyo alikabidhi Sh.200, 000 kwa ajili ya nauli za walimu wa shule hiyo katika kipindi cha likizo  na Sh .600,000 kwa ajili ya mitihani ya Majaribio.

Wakati Sh.300, 000 zilitolewa na Azim Khan na Sh. 300, 000 zilitolewa na EMA Ilala Tobola.

Aidha vitu vingine ambavyo wameaidi kupeleka mwisho wa mwezi huu EMA Ilala  ameaidi mashine ya photocopy na Azim khan Compyuta.

Kuhusu suala la changamoto ya ukuta wa shule ameahidi kutafuta wadau waweze kutatua tatizo hilo.Pia atazungumza na Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema na mkurugenzi wa Ilala.

” Nampongeza Azim Khan kwa msaada huu mkubwa na mimi kama EMA wa Ilala ndio mlezi wenu naomba mnishirikishe vikao na walimu nipate muda wa kuzungumza nao niweze kujua changamoto zao naitaji taaluma iwe juu shuleni hapa,hivyo kama walimu wangu nitakuwa nao pamoja” amesema.

Kwa upande wake Azim Khan amesema anatekeleza Ilani ya chama katika kukuza taaluma shuleni  ili baade wapatikane wanafunzi bora.

Khan amesema jukumu la kusaidia sekta ya elimu ni la kwetu sote sio kuiachia serikali  .

” Tunaungana na serikali yetu pendwa  ya Ilala kumsaidia Rais Magufuli na Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema kuakikisha taaluma inapanda katika shule za msingi zilizopo wilayani  Ilala” amesema Khan.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mchikichini Wilson Mahemba amesema shule hiyo ina idadi ya walimu 23 na wanafunzi 503 kati yao wavulana 253 na wasichana 250.

Katibu wa Elimu  Malezi na Mazingira Wilaya ya Ilala  (EMA) Wilison Tobola akiwa na wajumbe wake Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi vifaa vya Shule katika shule ya msingi Mchikichini Dar Es Salaam leo  vyenye thamani ya 700,000 vilivyotolewa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu (CCM ) Mkoa Dar es Salaam Azim Khan (Kushoto) Kulia Mwalimu mkuu wa shule hiyo . Wilson Mahemba ( Picha na Heri Shaban)Read More

Share.

About Author

Comments are closed.