Thursday, August 22

DK ABBAS AZUNGUMZIA UMUHIMU MAOFISA HABARI KUTOA TAARIFA

0
Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii
MSEMAJI wa Serikali Dkt. Abbas Hassan amesema utoaji taarifa na habari kwa sasa ni takwa la kisheria na si utashi wa ofisa habari na tayari wameelezwa hilo na wanaliambua.

Dk.Abbas ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya Shirika lisilo la kiserikali la Twaweza kutoa matokeo ya utafiti mpya wa mwaka 2018.Utafiti huo umetolewa leo jijini.

Amesema utafiti huo umeonesha namna ambavyo wananchi wametoa maoni yao katika suala la upatikanaji wa taarifa nchini na kufafanua kwa sasa suala la kutoa taarifa ni takwa la kisheria.

“Tunayo sheria sasa ambayo inatoa ulazima wa taarifa kutolewa pale inapohijika.Kutoa taarifa ni hatua moja lakini pia lazima tuangalie sasa hiyo habari ikoje katika suala la usalama wa nchi.Kwa upande wetu wote ambao wanahusika na utoaji taarifa wanajua ni wajibu wao na lipo kisheria,”amesema Dk.Abbas.

Amesema wananchi wengi wanaamini na kusikiliza au kupata habari kupitia redio na kwamba mchango wao kama Serikali wanao mchango wao na kwamba hadi jana inaonesha magezeti na majarida, machapisho ambayo yamesajiliwa ni 169 ambayo yamesajiliwa na redio 150 ambazo zimepewa leseni.

Amefaanua wanatoa kipaumbele kwenye maendeleo ya redio na kwamba wamejikita katika kutoa mafunzo mbalimbali.Kuhusu maofisa habari amesema  dhana nzima ya utoaji habari na taarifa zi lazima uvae suti na kufafanua kwa sasa kwa ofisa habari kutoa habari si utashi binafsi bali ni takwa la kisheria

Amepongeza utafiti wa Twaweza na kusisitiza uwe endelevu kwa kufanyika hata kila baada ya miezi sita.Pia sheria zifuatwe na kuhusu suala la uhuru wa habari ameeleza kuwa ni muhimu lakini uzingatie haki na wajibu wake.


“Kikubwa tufahamu sisi wote ni wadau na hivyo tushirikiane na kwamba kikubwa ni kupigania haki ya kupata habari.Kuna taratibu za kufauata na hata pale unaposikia kuna haki ya kuishi lazima ufurukute ili uishi.Nashauri mambo mengi kuhusu masuala ya habari na hilo ndio kazi yangu,”amesema Dk.Abbas.

Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe(ACT WAZALENDO) amesema kwa mujibu wa utafiti watu wengi wamesema hawajisii kumkosoa Rais, Makamu wa  Rais na Waziri Mkuu.

Pia utafiti unaonesha wananchi wengi hawaamini taarifa mbalimbali ambazo zinatoka kwenye vyanzo mbalimbali na hivyo iko haja ya watoa taarifa hizo zitazamwe na kufafanua huenda jamii inaona habari zinazotoka hata kwenye vyombo vya habari si sahihi.

Amesema utafiti unaonesha kuwa wananchi wengi sasa wanamini zaidi matamko ya Rais na Waziri Mkuu na kuomba Twaweza kuagalia mbunge wa Kigoma mjini amepongeza taasi hii na ameshauri kuwe na ulinganifu kwa kuangalia huko nyuma kulikuaje.

“Tunapaswa kupata ulinganifu wa kimuda ambao haujafanyika kwenye utafiti na kwamba anamini huko mbele wataonesha na ulinganifu kati ya mwaka mmoja na mwingine kwa yale ambayo wanayafanyia utafiti,”amesema.

Akizungumzia utafiti huo Mkurugenzi wa TWAWEZA Aidan Yakuze ameeleza utafiti huo kati ya mambo ya waliyoangalia ni uhuru wa kumkosoa Rais, makamu wa Rais na waziri mkuu ambapo matokeo yameonesha kuwa  wananchi hawajisikii huru kumkosoa Rais kwa asilimia 60, Makamu wa Rais asilimia 54 na Waziri mkuu asilimia 51.

Pia utafiti huo unaonesha wananchi hawapo huru kuwakosoa Mawaziri kwa asilimia 47, wakuu wa mikoa asilimia 46, na Wakuu wa wilaya kwa asilimia 43.

Aidha utafiti huo umeonesha kuwa wananchi wengi wana imani kubwa na taarifa zitolewazo na Rais kwa asilimia 70, na Waziri mkuu asilimia 64.

Pia kwa upande wa wawakilishi wabunge wa Chama tawala kwa asilimia 26, wabunge wa upinzani  asilimia 12, viongozi wa serikali asilimia 22 huku idadi ndogo zaidi wanawaamini Wenyeviti wao wa vijiji kwa asilimia 30.

Pia utafiti huo umeonesha kwamba uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari unaungwa mkono na wananchi walio wengi wao kwa asilimia 62 wameeleza kuwa gazeti lililochapisha taarifa za uongo ama zisizo sahihi liombe radhi na kuendelea kuchapisha.

Aidha utafiti huu umeonesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi hawafahamu sheria mpya zinazosimamia masuala ya taarifa hasa za kimtandao na zile za kitakwimu.
 Mbunge wa kigoma Mjini Zito Kabwe akizungumza na waandishi wa Habari akiwapongeza Taasisi ya Twaweza kwa kazi nzuri walioifanya,akiwataka wasiishie mjini tu waende na vijijini.
 Msemaji Mkuu wa Serikali Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa Habari Mara baada ya kupokea ripoti hizo kutoka kwa Twaweza,na akiwataka kufanya tafiti hizo kuwa endelevu kwa kila Baada ya miezi 6 Leo katika makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza Aidan Yakuze akizungumza wakati wa kutoa ripoti ya namna ya uwasilishwaji wa Taarifa na habari kwa Jamii leo makumbusho ya Taifa Jijini Dar ea Salaam.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.