Monday, August 26

DC AKATAA NYUMBA YA WALIMU YA MILION 52-SCRIPT PICHA NA SAUTI

0


 Na Ahmed Mahmoud Karatu

Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo amegoma Kupokea Nyumba ya walimu ambayo inadaiwa kugharimu shilingi Milioni 52, zikiwa ni fedha kutoka kwa wafadhili milioni 34, nyingine zikitolewa na wananchi pamoja na serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu amefikia hatua hiyo wakati akipokea majengo mengine mawili ya bweni la Wanafunzi wa Kike pamoja na bwalo la Chakula yaliyojengwa na kwa ufadhili kutoka The African Foundations.

Huku akikaata nyumba ya walimu ya 3 in one ambayo imefadhiliwa na
Serena hotel kwa madai fedha zilizotumika haziendani na uhalisia wa
mradi.

Katika mradi huo, Wananchi wameoa kiasi cha milioni Tisa, huku
serikali ikitoa pia milioni Tisa kwaajili ya upauzi wa jengo.

Kwa upande wao wafadhili wa mradi huo wamekiri uwepo wa mapungufu hayo
na kuahidi kuyafanyia Kazi.

Kuhusu msaada wa ujenzi wa Bweni la Wasichana pamoja na Bwalo la
Chakula, Mkuu wa wilaya Mahongo amepongeza ujenzi huo, huku Meneja wa
African Foundation, Mkomeni Ernest, amasema lengo ni kuhakikisha jamii
inanufaika na uwepo wa makampuni yanayozunguka hifadhi zilizo karibu
na wananchi.

Share.

About Author

Leave A Reply