Friday, August 23

DAWASCO YATOA ONYO, WEZI WA MAJI MAGOMENI

0


Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
MENEJA wa Shirika la Maji safi na maji taka  (DAWASCO) Magomeni Mponjoli Damson ametoa rai kwa wateja wanaounganisha maji kiholela kupitia mita za DAWASCO kuacha mara moja. 

Akizungumza na waandishi wa habari Mponjoli ameeleza kuwa wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakiiba maji kutoka mita za DAWASCO kwa kutokujua au kwa makusudi kabisa kwa maslahi yao binafsi hali inayohatarisha usalama wa mita hizo na kukosa maji wa baadhi ya wakazi wa maeneo hayo.

Amewataka wananchi kutounganisha maji kwa mtu mwingine kupitia mita za mamlaka hizo na kuacha mamlaka husika kufanya kazi yake na kuweza kutoa huduma wa wakazi wote.

Aidha Mponjoli ameeleza kuwa changamoto hii inatokana na wakazi wengi kukosa elimu  kuhusu huduma za kuunganisha maji na kama mamlaka wapo tayari kutoa elimu kwa wananchi wote.

Aidha mponjoli ametoa wito kwa wakazi wa Magomeni kuuliza kwa mamlaka husika kuhusu huduma za kuunganishiwa maji kutoka kwa mamlaka husika sio mteja wa kawaida.

Ameeleza kuwa kama mamlaka wapo tayari kutoa elimu kwa wananchi na kushauri namna ya kuunganisha maji kama inavyostahili sio kiholela.

Mwisho ametoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na mamlaka hayo na zikikiukwa lazima sheria zifuate mkondo wake kwa kulipa faini na hatua nyingine za kisheria.
Meneja wa Shirika la Maji safi na maji taka (DAWASCO) Magomeni, Mponjoli Damson akionesha moja ya pampu za maji walizozikamata kwa wateja waliounganisha maji kiholela kupitia mita za DAWASCORead More

Share.

About Author

Comments are closed.